Home Kimataifa Daftari la Zahera na Kakolanya lisomwe na vilabu na wachezaji wote Tanzania.

Daftari la Zahera na Kakolanya lisomwe na vilabu na wachezaji wote Tanzania.

4765
0

Makala na Raphael Lucas
Matatizo ya kinidhamu na kiutawala yaliyoikumba klabu ya Yanga msimu huu yanatakiwa kua kama kituo cha kujifunza kwa viongozi na mashabiki kwa ujumla

Suala la Yusuph Manji
hili ni Suala na tatizo kubwa la kiutawala lililoikumba Yanga baada ya mwenyekiti wao kutangaza kujiuzulu na kuiacha timu katika wakati mgumu kutokana na mfumo wa Yanga kumtegemea zaidi Manji kiutendaji hasa kwenye kujitolea hela za usajili na malipo ya mishahara pasipiokua na mbinu mbadala za kutengeneza vyanzo vya kipato vya klabu kwa ujumla

Suala la Kakolanya
Hapa wachezaji wote hasa wa Kitanzania wanapaswa kujifunza jinsi ya kudai maslahi yao pasipo kuvunja utaratibu, kwani Kakolanya alikua anadai malimbikizo ya mshahara na malipo ya usajiri wake lakini yeye aliamua kukaa nyumbani ili adai malipo ambalo ni kosa kisheria.

Nidhamu ya Zahera
Zahera ni kocha aliyejipambanua hasa kuamini katika kujenga nidhamu za wachezaji kwani amewahi ingia kwenye matatizo ya kinidhamu na wachezaji Beno, Yondani na Ajib ambaye kwa sasa amebadilika kinidhamu kiasi kwamba Zahera kumwamini na kumpa kitambaa cha unahodha.
Yaliyopita hasa kwa wana Jangwani tujaribu kujifunza kwani ni somo tosha kwa soka letu lililojaa makando kando ya matatizo

Raphael Lucas (udom)
0710690782/0764764449

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here