Home Kimataifa Cristiano Ronaldo – Mgodi unaotembea – hivi ndivyo timu pinzani Serie A...

Cristiano Ronaldo – Mgodi unaotembea – hivi ndivyo timu pinzani Serie A zinavyomtumia kibiashara

13968
0

Ilifahamika wazi kwamba kuwasili kwa Ronaldo Serie A kungeongeza demand ya mambo mbalimbali nje na ndani ya uwanja.

Siku moja baada ya uhamisho wake kutoka Real Madrid kutangazwa iliripotiwa Juventus waliuza jezi zaidi ya laki 5 ndani ya masaa 24 tu. Tiketi zote za msimu za Juventus ziliuzwa ndani ya wiki moja tu.

Achana na faida ambazo wanaendelea kuzipata Juventus sasa wapinzani wao nao wameanza kumtumia CR7 kuongeza mapato yao.

Imeripotiwa klabu ya Parma ambayo itacheza mechi ya 3 ya ligi vs Juventus msimu ujao katika uwanja Stadio Ennio Tardini, imepandisha kwa kiasi kikubwa tiketi za mchezo huo.

Kwa mujibu wa Tuttosport, siti za kaskazini mwa uwanja huo ambazo kwa kawaida huwa zinagharimu kiasi cha €25 lakini sasa zitagharimu kiasi cha €178 (kutoka elfu 66,000 mpaka 475,000) kwa mechi moja tu.

Msimu uliopita tiketi ya msimu mzima ya Parma katika eneo hilo la uwanja ilikuwa inaagharimu kiasi cha €190 – sawa na laki 507,00.

Bei hizi zimepanda maradufu zaidi katika maeneo mengine ya uwanja. Tiketi ya ambayo ilikuwa inagharimu kiasi cha 161,000 kwa mchezo sasa inagharimu 531,000 (€60 – €199), tiketi ya €70 sasa itauzwa €233 (kutoka 186,000 mpaka 622,040) na tiketi ya €100 imefika €386 (267,000 mpaka kufikia millioni 1.1).

Tiketi ya juu kabisa ya msimu ya Parma msimu uliopita ilikuwa inauzwa €150 na sasa inauzwa €450 – kutoka laki 4 za kitanzania mpaka kufikia millioni 1.2.

Wanachokifanya Parma ndio ile waswahili wanasema mgeni njoo wenyeji tupone!

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here