Home Kimataifa Comoros watinga mahakamani kuishtaki Cameroon

Comoros watinga mahakamani kuishtaki Cameroon

2336
0

Taifa la Comoros limefungua kesi kwenye mahakama ya usuluhisho ya soka kwa ajili ya kuomba Cameroon watolewe katika michuano ya mataifa huru ya Afrika.

Cameroon wapo kundi moja na Comoros wanatarajia kukutana mwezi machi.

Mkurugenzi mkuu wa shirikisho al soka nchini Morocco ameilaumu CAF kwa kushindwa kutimiza mojawapo ya wajibu wake ambao unaoatika katika ibara ya 92.3

Sheria inasema kuwa timu ikiondolewa kwenye mashindano inapaswa kulipa faini ya dola 500 000 na itapigwa marufuku kushiriki mwaka unaokuja.

Comoros wamesema kuwa kitendo cha Cameroon kunyang’anywa haki za kuandaa kombe hilo basi hata nafasi yake ya kufuzu moja kwa moja inapaswa iondolewe pamoja na adhabu.

Comoros wana alama 5, Cameroon wana alama 8, Morocco wana alama 10

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here