Home Kimataifa Chilunda atolewa kwa mkopo Hispania

Chilunda atolewa kwa mkopo Hispania

5221
0

Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Shaabani Idd Chilunda ametolewa kwa mkopo na klabu yake CD Tenerife kwenda Club Deportivo Izarra kwa kifupi CD Izarra hadi mwishoni mwa msimu huu.

Chilunda alikuwa hapati nafasi mara kwa mara kwenye kikosi cha Tenerife tangu alipojiunga na klabu hiyo mwaka uliopita.

Izarra inashiriki Segunda Division B (Second Division B) ligi ya tatu kwa mumo wa soka la Hispania juu yake kuna Segunda Division (ambako alikuwa na Tenefire) halafu juu ndio Primera Division au kwa jina jingine La Liga.

Kwa maana hiyo timu inayoshiriki Segunda Division B ikipanda daraja inakwenda Segunda Divion halafu ndio La Liga lakini ikishuka kutoka Segunda Division B inaangukia kwenye ligi chini zaidi inayojulikana kama Tercera Divion.

Segunda Division B ligi ambayo atakuwa anacheza Chilunda kwa sasa inajumuisha pia wachezaji wa reserve kutoka baadhi ya timu za La Liga pamoja na Segunda Division.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here