Home Ligi BUNDESLIGA CHICHARITO AZUNGUMZIA HATMA YA VAN GAAL OLD TRAFFORD

CHICHARITO AZUNGUMZIA HATMA YA VAN GAAL OLD TRAFFORD

718
0

Chicharito 2

Striker wa zamani wa Manchester United Javier Hernandez anaamini Louis van Gaal anaweza akafanikiwa akiwa Old Trafford licha ya kuwa na matokeo magumu msimu huu.

Siku za maisha ya maisha ya kocha Mholanzi Louis van Gaal pale Old Trafford zinahesabika huku kukiwa na presha kubwa kutokana na uvumi wa bosi wa zamani wa vilabu vya Chelsea na Real Madrid Jose Mourinho kuchukua mikoba yake itakapofika majira ya kiangazi zikizidi kuchukua sura mpya.

ChicharitoVan-gaal

Mshambuliaji wa Mexico aliyeikacha Manchester United na kujiunga na Bayer Leverkusen wakati wa usajili uliopita kufuatia kuachiwa na Van Gaal amesisitiza kuwa kocha huyo wa zamani wa Barcelona na Bayern Munich anaweza akafanya mapinduzi kwenye Premier League.

Hernandez ameiambia Sky Sport: “Ni kocha mzuri kiukweli. Anambinu zake kama walivyo makocha wengine duniani”.

Chicharito-vs-Club-Brugge

“Huwezi kumpata Sir Alex Ferguson mpya ndani ya miaka 50 au 100 kwasababu yeye ni wa kipekee. Alikuwa ni mtu maalumu”.

“Van Gaal anaweza akafanikiwa lakini kwenye soka muda na matokeo vitazungumza kama ni mtu sahihi kinoa United au la”.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here