Home Kitaifa Chama anatisha sana, Ajib ana mengi ya kujifunza

Chama anatisha sana, Ajib ana mengi ya kujifunza

5838
0

Hawa wote ni wachezaji wanaocheza ligi kuu Tanzania Bara. Pia wanacheza timu kubwa hapa nchini ambazo zina historia kubwa. Wote msimu huu wameonyesha kiwango kikubwa katika timu zao.


Bila shaka hawa ni washambuliaji ambao wamekuwa kivutio kikubwa sana.


Ibrahim Ajibu

Jukumu: Anacheza kama kiungo mchezeshaji au kiungo mshambuliaji. Amekuwa na ufanisi murua anapokuwa na mpira nyuma ya mshambuliaji.

Faida zake: Ni mwepesi kupiga pasi za mwisho ambazo mara kadhaa zimekuwa na madhara. Ana uwezo wa kuratibu mipango wa mpira mirefu. Akili yake ina uwezo wa kufanya kazi kwa haraka. Nidhamu yake ya kuhakikisha mpira unapaswa kufika eneo husika na kwa haraka. Ana uwezo wa kufungua macho na kuona mbali.

Madhaifu: Ajib ni mvivu. Ni mzuri wakati timu ikiwa inashambulia. Timu ikiwa na mpira kwenye robo ya eneo la adai utauona uzuri wake. Ajib anapenda kutembea kuliko kukimbiam

Clautous Chota Chama

Kwa sasa yawezekana kuwa ndiye kiungo bora ligi kuu bara? Kwangu mimi jibu ni ndio. Chama hachagui shoo, ukimpa namba 8 anakamua, 6 anakamua 10 anakamua kufunga pia sio tatizo kwake.

Faida: Anajituma sana. Anajua alichoagizwa. Ana uzoefu mkubwa wa kucheza vilabu tofauti tofauti na vikubwa katika ligi ya Zambia na nje ya Zambia.

Madhaifu: Alichokosea Chama ni muda wake na sehemu aliyopo. Kwa ubora wake na kiwango chake alipaswa kuwa Afrika kusini. Sasa ana miaka 27 ya passport kimsingi hapo umri ushaenda mtu mzima yule. Madhaifu ya Chama inafaa kuwa elimu kwa wachezaji wa ndani. Yamkini labda alikosa menejementi nzuri. Au labda amekuja kuwa bora ukubwani. Au hakuwa nasoka la malengo. Kiwango chake kina zidi ubora ligi yetu.

Faida ya madhaifu yake ni onyo kwa wachezaji wetu. Chama miezi kadhaa tu ameonekana nyota. Wachezaji wetu wa ndani bado wapo wanaduwaa tu!

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here