Home DOKUMENTARI Carrick sio Paka ni simba aliyenyeshewa

Carrick sio Paka ni simba aliyenyeshewa

13139
0

Msimu wa 2006 tarehe 31 Mwezi Julai, Spurs walipokea dau la £14m, kumuuza Carrick, kuelekea klabu ya Man United. Ilikuwa tarehe kama ya leo na mwezi kama leo ndipo Carrick alielekea Old Trafford.

“Nakumbuka wakati Michael anakuja alipewa jezi namba 16 shirt jezi iliyovaliwa na Roy Keane, moja ya viungo bora kuwahi kutoka katika ligii kuu England (Premier League). Nilimuonea sana huruma kwa sababu alikuwa ananonekana mpole na nilidhani viatu alivyopewa ni vikubwa mno kwake. Nilipenda tabia yake mazoezini na uwanjani. Najivunia kucheza nae pamoja. Nilikiwa naajiona huru sana uwanjani kama Carrick yupo.

Kuwa nae katikati nilikuwa kwenye mikono sahihi zaidi. Navhokidhania ni kwamba ile heshima anayopewa Carrick haiendani hata kidogo na ushujaa wake. Kila ninapomuona Michael uwanjani, nafsi yangu inasuhuzika maana najua United ushindi hapo asilimia kubwa. Carrick kwangu ni sawa Rolls Royce, iliyokuwa inazunguka uwanjani.” Haya ni maneno ya Paul Scholes

Mpira wa kiingereza ni mgumu sana. kwanza ni mgumu kwa aina ya uchezaji na ni mgumu kwa mchezaji kufanikiwa na kuimbwa. kuna mtu kama Lee Barry Cattamole, akiwa na umri mdogo kabisa wa miaka 19 tu na siku 47 alikuwa nahodha ya klabu ya Middlesborough lakini nani anayemjali sana wakati yupo timu inayoshabikiwa na mji tu?

“Wakati nacheza England nilikosa bahati ya kucheza na mtu kama Carrick, ni mshapu wa maamuzi wala hajazubaa uwanjani.” Xabi Alonso

Unapokuwa unaangalia mpira wa kiingereza utamu wake ni vurugu vurugu za akina Roy Keane, viatu vya akina Barry, Claudio Makelele ya akina Steven Gerrad, Hasira za akina Wayne Rooney, uchokozi wa akina Joe Barton na mashuti ya akina Frank Lampard. Lakini wapo watu wawili walijificha kwenye kivuli cha soka la Uhispania na wengi hawakujali sana kazi yake. Anaitwa Michael Carrick.

“Carrick alipaswa kucheza Barcelona; Nadhani huyu ni mchezaji asiyeongelewa sana hapa England.”
Arsene Wenger

“Carrick ni mmoja kati ya viungo wachezeshaji na wazuiaji bora duniani ambao pia nimewahi kuwaona. Napenda kumfananisha na Xabi Alonso, Sergio Busquets .” Pep Guardiola

Sergio Busquets ni mmoja ya viungo ambao pia wanaweza kuonekana kuwa wadhaifu. Lakini huyu ndiye chachu hasa kupata ubora halisi wa Xavi na Andrés Iniesta. Hawa wote walicheza kwa uhuru wakijua kuwa Sergio anamaliza kila kitu. Wakati Busquets anasajiliwa na Guardiola wemgi walimdharua lakini kwa sasa wamegundua kuwa mpira sio miguvu pekee.

Ni ngumu kumpoteza Carrick au Busquets na Xabi Alonso. Carrick ndiye mchezaji pekee aliyeonekana kucheza vyema kwenye fainali ya UEFA 2011 kayi ya wachezaji wote wa Man United wapokutana na Barcelona ndani Wembley dhidi United.

Dimba la katikati la Engand limewapoteza akina Lampard na Gerrard, kisha Michael Carrick amefuatana na Scott Parker.

“Carrick anaipa Man United nyenzo nzuri ya kufanya timu itulie vyema katika pande zote, anapiga pasi nzuri, anapika magoli na ana upeo mzuri sana.” Xavi Hernandez

Hupaswi kukata tamaa katika maisha. Mwaka 2000/01, alifanikiwa kucheza michezo 41 ilikuwa kwa mara yake ya kwanza kwa kipindi cha miaka minne katika ligi la daraja la kwanza. Msimu wa 2003/04, alichaguliwa kwenye timu bora ya msimu.

Carrick aliondoka West Ham baada ya klabu hiyo kushuka daraja na alielekea upande wa pili wa London kwenye klabu ya Tottenham Hotspur. Hapo ndipo alipo mshawishi kocha mkuu wa Man United Sir Alex Ferguson.

“Michael ni sawa Scholes wachezaji hawapendelei sana umeaarufu. Sio kwamba hajui umuhimu wa umaarufu ila ni tabia yake tu miaka ya nyuma pia alikiwepo Denis Irwin alikuwa hivyo hivyo pia. Michael anachokiangalia ni timu inataka nini na sio yeye anataka nini. Alijaliwa akili nyingi sana nje na ndani ya uwanja. Na nadhani huyu ndiye kiungo wa kati bora zaidi hapa Uingereza kwa sasa (2014)”
Sir Alex Ferguson

Changamoto aliyokumbana nago Carrick ni kwamba waingereza walimthaminisha kiungo mkabaji katika picha ya Claude Makélélé. Kwamba kama hutumii nguvu, hukabi kwa kucheza rafu na ubavu basi wewe kwao ni kiungo mkabaji dhaifu

“Ukitaka kujua Michael ni nani cheza nae na pia cheza dhidi yake” Ryan Giggs

Wachezaji wa dimba la kati England usipocheza rafu wewe kwao sio bora. Mimi naona hayo ni mawazo mgando tu. Parker huyu ndiye aliyempa Modric uhuru wa kutawala dimba la juu kwa amani. Sura ya Parker ilijificha kwenye maumbile ya akina Sergio Basquet, Marehemu Cheik Tiote, Alexandra Song, Carrick na Steven Gerrard. Wayne Roonye pia alifaidi sana mabawa ya Michael Carrick.

Aliposajili kutoka West Ham na kwenda Tottenham, alionekana kama Paka kwenye kundi la mbwa kumbe ni Simba aliyenyeshewa.

“Carrick sio mchezaji wa msimu. Wengi wetu tunawapenda. Wale wachezaji wa magazetini kuliko uhalisia. Carrick ni noma.” Thierry Henry.

Hao walionekana kwa sababu timu zao zilikuwa na mashabiki wengi na zilipata mafanikio ambayo yaliwapa heshima kubwa. Ni aina ya kiungo ambaye sio lazima acheze rafu nyingi.

Kwa miaka ijayo sijajua nani atavaa viatu vya Carrick ukiachilia mbali Gerrard. Sio Man United tu hata timu ya taifa ya England simuoni Carrick kwenye kivuli cha Eric Dier. Dier anatumia sana nguvu kuliko akili kama Carrick.

“Michael Carrick alikuwa kiboko ya Liverpool, Arsenal na Manchester City, tena usiombe awepo Scholes utagundua nachokisema. Ukimwangalia Carrick anavyocheza ni sawa na kwenda baa ambayo kuna piano pembeni inapigwa. Carrick ni piano.” Gary Neville

“Harry, Michael Carrick huyu ni kiungo bora kuwahi kumuona kwa macho yangu. Carrick namuona kwenye picha ya Glenn Hoddle.’” Harry Redknapp

Kwaheri Carrick

Usiache kufuatilia dauda Tv kwenye yotube Channel. Mimi Privaldinho (Instagram)

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here