Home Kimataifa Boston Celtics Ya Mtu Mfupi Yamnyemelea Lebron James Fainali.

Boston Celtics Ya Mtu Mfupi Yamnyemelea Lebron James Fainali.

2384
0

Inawezekana kimo chake kikawa sababu kubwa ya klabu ya Sacramento Kings kuamua kuachana nae lakini ameweza kupageuza Boston Celtics nyumbani na ndiye nyota ama staa wa timu hiyo kwa sasa. Anaitwa  Isaiah Thomas na alicheza kwa mara ya kwanza kwenye maisha yake mchezo wa 7 wa hatua ya mtoano ambao alikiri kuwa tofauti na wengi walivyodhania yeye hakuwa na presha yoyote.

Alicheza tofauti na siku zote katika mchezo huo wa 7 dhidi ya Washington Wizards ambao ulikuwa wa nusu fainali na aina yake ya mchezo ilimpa nafasi mchezaji Kelly Olynyk kutokea benchi kwa upande wa  Boston Celtics na kufunga pointi 26 ambazo zikaifanya Celtics kushinda dhidi ya Washington Wizards kwa pointi 115-105.

Thomas alimaliza mchezo akiwa na pointi 29 na pasi 12  na sasa wanaelekea katika fainali za kanda ya Mashariki dhidi ya klabu inayopewa nafasi zaidi ya Cleveland Cavaliers ambayo ina mchezaji bora zaidi kwenye ligi katika jina la Lebron James.

“Nilifahamu ungekuwa mchezo mkubwa sana usiku wa leo, nilifahamu usingeweza kuwa mchezo rahisi hata kidogo,” Thomas alisema. “Na tulifanikiwa kuondoka na ushindi.”

Boston wanaingia kwenye fainali ya kanda ya Mashariki ambayo wataikaribisha Cleveland Cavaliers katika mchezo wa kwanza wa fainali usiku wa Jumatano kuamkia Alhamis. Itakuwa ni mara ya kwanza kwa Celtics kuingia fainali ya kanda ya Mashariki tangu mwaka 2012.

“Huu utakuwa wakati wa kipekee kwa sababu tumepata nafasi ya kukutana na Cleveland Cavaliers katika fainali,” alisema kocha wa Boston Celtics Brad Stevens.

Bradley Beal aliiongoza Wizards kwa kufunga jumla ya pointi 38 ikiwemo pointi 24 katika kipindi cha pili. Washington Wizards walikuwa wakicheza mchezo wa kwanza wa 7 kwenye hatua ya mtoano tangu mwaka 1979.

Otto Porter aliongeza pointi 20, John Wall na Markieff Morris kila mmoja alifunga pointi 18. Lakini Washington walipoteza mipira (turnovers) mara 15 iliyopelekea pointi 17 za Celtics.

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here