Home Kimataifa Bondia Mtanzania apongezwa Bungeni

Bondia Mtanzania apongezwa Bungeni

8245
0

Bondia mtanzania Hassan Mwakinyo aliyempiga bondia wa Uingereza Sam Eggington katika pambano la utangulizi kabla ya pambano kuu kati ya Amir Khan dhidi ya Samuel Vargas, leo amepongezwa na serikali Bungeni.

Pongezi hizo zimetolewa jijini Dodoma na Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dr. Harrison Mwakyembe.

“Nielezee kidogo kwa yaliyotokea Uingereza usiku wa kuamkia jana kwa mtanzania mwenzetu Hassan Mwakinyo wa Tanga kwa ushindi mnono alioupata huko Birmingham baada ya kumchakaza mwanamasumbwi nyota Sam Eggington katika raundi ya pili kati ya raundi 10.”

“Kabla ya pambano hilo kufanyika bondia wa Uingereza Sam Eggington alikuwa namba 8 kwa ubora duniani (kwa uzito wao) kati ya mabondia 1854 wakati Mwakinyo alikuwa ni bondia namba 174 na sasa hivi baada ya matokeo hayo, Mwakinyo ni bondia namba 16 duniani na wa kwanza Afrika na Tanzania.”

“Tunachukua hatua kuhakikisha kwamba vijana wetu wanaofanya vizuri katika michezo duniani tunawatambua na tunaendeleza vipaji vyao. Baada ya muda tutawakusanya wote kuweza kuchangia maendeleo ya michezo nchini.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here