Home Kitaifa Bodi ya ligi yakanusha upangaji matokeo

Bodi ya ligi yakanusha upangaji matokeo

2849
0

Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Steven Mguto amesema suala la upangaji matokeo hakuna kwenye ligi kuu Tanzania bara.

Mguto pia amekiri kuwepo kwa changamoto ya mechi nyingi za viporo huku Simba ikiwa ndio klabu yenye viporo vingi kwenye ligi hadi sasa.

“Ratiba kubadilika na timu nyingine kuwa na mechi nyingi za viporo ni kutokana na mashindano ya CAF lakini pia CAF wamebadilisha kalenda yao iendane na ya FIFA katika hali hiyo vitu vingi vimekuja kwa kufuatana.”

“Hatujapenda kuweka viporo ili timu nyingine ifaidike hapana, nafikiria timu yenye viporo ndio inaumia zaidi ya ile iliyocheza kwa sababu anakupa presha ya kushinda mechi zako ili umfikie.”

“Hili la viporo tunaliangalia kwa upande mwingine kwa sababu kuna watu wanahisi kuna kuwa na upangaji matokeo japo sisi hatuamini hivyo lakini kitu kikisemwa huwezi kukaa kimya lazima ufatilie.”

“Kwa hiyo sisi tunafatilia mechi zote kwa kupeleka watu wetu kufatilia kuona timu zinapata matokeo kwa haki. Suala la upangaji matokeo hakuna.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here