Home Kimataifa Beki mpya wa Simba aliachwa huru na Asec Mimosas?

Beki mpya wa Simba aliachwa huru na Asec Mimosas?

8754
0

“Msimu tulimuona kwenye mechi za awali akiwa anaanza kikosi cha kwanza. Baadae mwalimu Siaka Traore akamtumia Christian Angbandji ambaye alikuwa akiuguza majeraha. Lakini msijali sana Zana ni mchezaji mzuri sana. Kama mmefanikiwa kumsajili basi atawasaidia” Haya ni maneno ya Abdoul Koppa mwandishi wa jarida la sportsmania la nchini Ivory Coast nilipofanya nae mazungumzo.


Zana alizaliwa mwaka 1992 mwezi august tarehe 27. Ni raia wa Burkina Faso


Nilipatwa na mkanganyiko kutoka kwa vyombo vya habari hapa nchini ambazo zilizoripoti Zana amesajiliwa kutoka kwa Asec Mimosas.

Zana ametokea wapi?

COULIBALY Zana Oumar alisajiliwa na ASEC Mimosas July 2017. Alisajiliwa na Asec akitokea klabu ya African Sports. Kabla ya hapo Zana alikuwa nchini Romania alipokwenda kwa ajili ya majaribio.

Msimu wake wa kwanza alicheza mechi 12 za ligue 1, na Mechi 4 za kombe la shirikisho la Africa. Msimu wake wa kwanza Alifanikiwa kutoa assist 1 na kutengeneza takribani nafasi 5 za magoli katika michezo 12 hiyo.


Kiwango chake?

Beki huyo alicheza Asec mwaka mmoja pekee. Kwa mujibu wa kocha msaidizi wa Asec bwana N’GUESSAN Fabrice ameniambia kiwango cha Zana ni kikubwa na ni mchezaji anayejituma sana.

“Nilimuona Mchezo wa kwanza April 17, 2018, tukicheza dhidi ya CR Belouizdad kwenye mechi ya marudiano ya kombe la shirikisho Zana alionesha kiwango cha hali ya juu sana, alionesha ukomavu na upambanaji wa kipekee” Mwalim Fabrice.

“Kabla hatujampa nafasi ya kucheza niliongea na nahodha wa timu KOUTOUAN Akassou nikamwambia amweleze Zana kuwa Christian Angbandji ni majeruhi na tunamtegemea yeye kwa sasa” alielezea kocha huyo msaidizi.


Mchezo wa pili Christian bado alikuwa majeruhi na nyota wa zamani Bakary Kone ambaye ni mkurugenzi wa ufundi aliomba Zana kupewa nafasi tena ili aweze kuthibitisha uwezo wake.

Alicheza mchezo wake wa pili May 16, 2018, ndani ya uwanja wa Stadium of Martyrs Complex, ASEC Mimosas walikufa bao (3-1) kutoka kwa Vita Club ya Congo. Licha ya kichapo kile Zana alionesha uwezo mkubwa sana na hakuna bao lililotokea upande wake


Changamoto alizokumbana nazo?

Katika kikosi cha Asec Zana alikumbana na ushindani mkubwa wa nafasi kutoka kwa ANGBANDJI Alex na DENIS Kouao Damsen ambao wote walikuwa wakicheza kama namba 2.

Ugumu wa nafasi ulimnyima muda mwingi wa kucheza. Mwezi wa 8 mwaka huu Asec ikaamua kumwachia huru.

Coulibaly alikaa kwa kipindi cha miezi miwili bila klabu akiwa kama mchezaji huru. Klabu ya Williamsville mnamo 4/10/2018 ilimtambulisha kocha wao mpya Rachid Ghaflaoui raia wa Morocco na siku hiyo hiyo Williamsivile na Zana nae alisajiliwa na klabu hiyo.


Vyanzo vya habari hizo?
Kwa mujibu wa jarida la sportsmania la nchini Ivory Coast lilitoa chapisho mnamo tarehe 4 mwezi wa 10 mwaka huu likielezea kuwa makamu wa raisi wa klabu ya Williamsville bwana Lamine Diaby amemkaribisha Zana katika klabu hiyo. Mchezaji huyo alionekana akiwa na jezi ya klabu hiyo.

Istoshe katika katika ukurasa wa Williamsville wa Facebook mnamo tarehe 5 walithibitisha usajili wa Rachid na Zana.

Kwa kuongezea jarida la Fratmat la nchini humo mwezi novemba 6/2018, lilitoa taarifa kuwa klabu ya Asec Mimosas ipo njiani kuwanasa wachezaji kadhaa ili kuziba nafasi ya mshambuliaji Glodoueue Angel Bares na beki wao wa pembeni Zana Coulibaly ambao waliachwa huru na klabu hiyo wakati wa dirisha la usajili.

Beki huyo alisaini mkataba wa miaka miwili na Williamsville kabla hajanaswa na miamba ya soka Tanzania wekundu wa msimbazi. Lakini hakubahatika kuichezea WAC mpaka anasajiliwa na klabu ya Simba. Taarifa kupitia Zoonesport zinaeleza kuwa Zana alishindwana na klabu yake mpya ya Williamsville kwenye maslahi binafsi.

Yote kwa yote karibu sana Tanzania bwana Zana na jisikie upo nyumbani.

Mchezaji kuachwa sio tatizo hata kidogo kwenye soka kwa sababu kila mchezaji ana mfumo wake na kila kocha ana mchezaji wake.

Naitwa Privaldinho

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here