Home Ligi BUNDESLIGA Bayern wanahitaji point 3 kuwa mabingwa – Neuer na Mönchegladbach wanaweza kuwa...

Bayern wanahitaji point 3 kuwa mabingwa – Neuer na Mönchegladbach wanaweza kuwa tatizo

661
0

FC Bayern München watashinda taji la Bundesliga leo endapo watafanikiwa kupata ushindi dhidi ya Borrusia Mönchengladbach katika uwanja wao wa nyumbani wa Allianz Arena.

 Umuhimu wa mechi hiyo unazidisha ugumu wa mchezo huo, Borussia sio timu nyepesi na ndio ilikuwa timu ya kwanza kuifunga Bayern msimu baada ya Manuel Neuer kuruhusu goli 3 katika wavu wake.

Kipa huyo namba moja wa Ujerumani ni moja ya makipa wanaogopewa hata na washambuliaji wakubwa duniani lakini amekuwa na mkosi dhidi ya Mönchengladbach. Mechi ya 15 ya ligi aliruhusu goli 3 dhidi ya timu hii na Bayern wakapoteza mchezo wa kwanza msimu huu.
 Msimu uliopita, Neuer tena alikutana na Borussia na akaruhusu magoli mawili ya ushindi wa timu hii yaliyofungwa na Raffael katika mchezo uliopigwa katika dimba la Allianz Arena, ikiwa ni mara ya 3 kwa Borussia Monchengladbach kuifunga Bayern katika historia ya Bundesliga.

Hii haikuwa mara ya kwanza kwa Neuer kupata taabu dhidi ya Gladbach, alipokuwa Schalke pia walimsumbua sana kama inavyoonekana kwenye video hii hapa👇

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here