Home Kimataifa Barca “Man United ni underdog, Juventus hatuwataki”

Barca “Man United ni underdog, Juventus hatuwataki”

4956
0

Jana King Lionel Messi Lapurga kama anavyojulikana kwa mashabiki wake ameisaidia klabu ya Barcelona kuifumua Lyon kwa jumla ya magoli 5-1 na kufuzu hatua ya Robo.

Fununu zimezuka kupitia jarida la AS kuwa nyota wa Barcelona na benchi la ufundi kuna baadhi ya vilabu wasingependelea kukutana nazo kwa sasa.

Ni heri wakutane na vijana wa Ole Gunnar au hata Iker Casillas na Porto yake kuliko Juventus inaongozwa na jemedari wa Vitan Cristiano Ronaldo mnyama mkali wa mwituni.

Takwimu za United vs Barcelona
10/11 Fainali: Barcelona 3:1 Man United
08/09 Fainali: Barcelona 2:0 Man United
07/08 Nusu: Man United 1:0 Barcelona
07/08 Nusu: Barcelona 0:0 Man United
98/99 Makundi: Barcelona 3:3 Man United
98/99 Makundi: Man United 3:3Barcelona
94/95 Makundi: Barcelona 4:0 Man United
94/95 Makundi: Man United 2:2 Barcelona

Kila mtu kwenye vyumba vya kubadilishia nguo kule Catalunya hawataki kabisa kusikia kuhusu Juventus au Guardiola.

Man City nayo imekuwa tishio siku za hivi karibu na Guardiola ana uchu mkubwa wa taji hilo.

Ajax, Liverpool na Spurs, wanafanya vizuri lakini Barcelona haiwezi kuzihofia timu hizo kama City na Juve.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here