Home Kimataifa Baada ya Pep kuchinjwa jana leo ni leo Vardy vs Salah

Baada ya Pep kuchinjwa jana leo ni leo Vardy vs Salah

3369
0

Liverpool vs Leicester City, mchezo huu utapigwa majira ya saa 23:00 kamili usiku katika dimba la Anfield stadium.


………Liverpool, ameshinda michezo yote mitatu ya mwisho kwenye ligi kuu England aliyokutana na Leicester City.mara ya mwisho Liverpool, kushinda michezo minne mfululizo ilikuwa mwaka 1987 na mwaka 1996.
.
.
………Leicester City, wamepoteza michezo sita kati ya michezo 7 ya ligi kuu England dhidi ya Liverpool sare (1) mara ya mwisho kupata ushindi Anfield, ilikuwa mnamo mwaka 2000 Kwa mabao 2-0.

.
.
………Liverpool, hajawahi kupoteza mchezo hata moja kati ya michezo 19 waliyocheza kati kati ya wiki kwenye ligi kuu England (Jumanne, Jumatano, na Alhamisi) ameshinda mara 13 na sare 1 tangu mara ya mwisho alivopoteza dhidi ya Fulham, kwa bao 1-0 mwaka 2012.
.
.
………Liverpool, hajapoteza mchezo hata moja katika michezo 32 ya ligi kuu kwenye uwanja wa nyumbani ameshinda mara 23 na sare 9.

.
.
………Liverpool, wanaangalia uwezekano wa kushinda mchezo wa nane mfululizo kwenye ligi kuu katika uwanja wa nyumbani kwa mara ya Kwanza mara ya mwisho kufanya hivo ilikuwa mwaka 2010.
.
.
………Leicester City, wamepoteza michezo 11 ya ligi kuu dhidi ya timu zinaongoza ligi kuu pia wameruhusu mabao 27 na wamefunga mabao 5.
.
.
………Andrew Cole, amewafunga Liverpool mabao (11), Thienry Henry (8), na Jamie Vardy (7).
.
.
Azizi Mtambo 15

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here