Home Kitaifa Azam yapigwa ‘pin’ Mlandizi

Azam yapigwa ‘pin’ Mlandizi

2808
0

Azam imelazimishwa suluhu na Ruvu Shooting kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara kwenyeuwanja wa Mabaini, Mlandizi-Pwani.

Kocha msaidizi wa Azam Juma Mwambusi amesema hali ya hewa ya jua kali imechangia matokeo hayo.

“Tulikuja na plan zetu lakini uwanja mbaya, sisi tumezoea kucheza mpira wa pasi na hiyo imekuwa ikitupa nafasi ya kuvunja mitengo ya timu yenye mipango ya kujilinda”-Juma Mwambusi, kocha msaidizi Azam FC.

“Ruvu wamekuja kukaba kwa nguvu kama ilivyo kawaida yao na tulilijua hilo lakini kwa sababu ya hali ya hewa (jua kali sana) tuliwaambia wachezaji watu wasicheze kwa kasi kwa sababu wangepoteza nguvu mapema.”

“Baadaye tukabadilisha plan tukawa tunapiga mipira mirefu na tukaweka viungo wawili pembeni kwa ajili ya kupiga krosi lakini hatukuwa na bahati.”

Mwambusi amesema Azam ilifunga goli halali lakini likakataliwa na waamuzi na hiyo inawezekana ni kutokana na waamuzi hao kuchanganywa na jua kali.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here