Home Kitaifa Azam wameanguka au wamejikwaa?

Azam wameanguka au wamejikwaa?

3883
0

Makala na Raphael LucasIvi ni kweli Azam jana ametoa suluhu na Ruvu shootings ya Masawe Bwire?Ni kweli Masawe Bwire anajutia kupata sare na timu kubwa Kama Azam?Pamoja na mpira kua ni fair play kutokana na matokeo wanayoendelea kupata Azam napata maswali mengi sana, najiuliza je Azam wamejikwaa ama wameanguka, baada ya hapo napata jibu na nabaki kukaa kimya.Wakati msimu wa ligi kuu Tanzania bara mwaka huu 2018/2019 unaanza Azam ilipewa nafasi kubwa sana kubeba ubingwa kutokana na aina ya usajiri wa wachezaji waliosajiri wakiwemo Donald Ngoma, Kutinyu na wengine wengi lakini kadri siku na michezo inavyoendelea Azam inazidi kua na wakati mgumu sana.Azam wamecheza mechi 18 na wanapointi 41 wakiwa nyuma ya Yanga kwa pointi 12 na tofauti ya mchezo mmoja huku Simba ikiwa nyuma yao kwa pointi 8 huku wakiw na viporo 4Kwa hesabu ya kawaida huwezi kusema Azam wameshaanguka bali wamejikwaa wanaweza inuka na kufuta mavumbi na kuanza safari. Hii ni kutokana na ligi kua bado mbichi japo changamoto zikizidi kuwaelemea ndivyo watapozidi kupata wakati mgumu kuwania ubingwa, Pamoja na Azam kua chini ya Hans van Pluijm na usajiri wa wachezaji Kama Chirwa aloongezeka kwenye dirisha Dogo bado wana changamoto kubwa ya matokeo.Imefikia hatua Azam nae imeanza kua club ya kawaida Kama zingine zilizowahi kuja na kujaribu kushindani na Simba na Yanga na mwisho wa siku zikapotea na kuuacha ufalme wa timu hizo mbili, Azam misimu mitatu iliyopita walikua tishio zaidi kuliko kadri siku zinavyoenda wanavyoendelea kupoteza ushindani wao mbele ya vilabu kongwe vya Simba na Yanga.Kutokana na hayo Azam wana jukumu kubwa la kuhakikisha wanarudi kwenye ushindani Kama walowahi kua nao wakati wa Stewart John Hall pamoja na mcameroon Joseph Omog hii sio kuishia kushika nafasi ya pili Bali kupata ubingwa Kama alivowahi fanya OmogRaphael Lucas(udom)0710690782/0764764449

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here