Home Kitaifa Azam vs Simba kufa au kupona

Azam vs Simba kufa au kupona

4330
0

Leo Ijumaa February 22, 2019 kuna mechi kali ya Azam vs Simba katika mwendelezo wa ligi kuu Tanzania bara itakayochezwa uwanja wa taifa kuanzia saa 10:00 jioni.

Maeneo manne ambayo yanaweza kuamua mechi ya leo ni matokeo ya mechi zilizizopita kwa kila timu, historia ya timu hizi zinapokutana, vikosi vya timu zote mbili pamoja na msimamo wa timu hizo kwenye ligi.

Matokeo ya mechi zilizopita

Azam wamedondosha pointi katika michezo mitatu ya iliyopita ya ligi kuu Tanzania bara. Simba imeshinda dhidi ya Al Ahly, ikashinda dhidi ya Mwadui kabla ya kushinda dhidi ya Yanga pamoja na African Lyon.

Geof Lea siku za hivi karibuni amewahi kusema, kikosi cha Simba kinaimarika kutokana na ushiriki wake kwenye michuano ya kimataifa ukiachilia mbali aina ya matokeo wanayopata. Ushiriki wao unawafanya kuwa kwenye maandalizi bora kuliko timu nyingine.

Historia timu hizi zinapokutana 

Tangu Azam imepanda daraja msimu wa 2008/09, imekutana na Simba mara 20 kwenye mechi za ligi kuu. Azam imeshinda mara 5 Simba imeshinda mara 9 kutoka sare mara 6. Timu hizo zimekutana mara 31 katika mashindano yote, Azam imeshinda mara 12,  Simba imeshinda mara 13 na kutoka sare mara 6.

Vikosi 

Azam ni miongoni mwa timu ambazo zinawachezaji wengi wa kimataifa, kikosi cha kwanza cha Azam kinawachezaji wasiopungua sita kutoka nchi tofautitofauti (Abarola, Kangwa, Wadada, Yakubu, Kutinyu, Ngoma, Chirwa, Agyei) kwa hiyo siyo timu ya kudharau.

Simba ilipumzisha nyota wake wengi katika mchezo dhidi ya African Lyon (Mkude, Kotei, Tshabalala, Chama, Dilunga) na wengine ambao walikuwa wanatumikia kadi ambao inawezekana leo wakacheza (Kagere, Okwi). Lakini ukizungumzia ubora wa vikosi, Simba inakikosi bora na kipana zaidi ya Azam. Mchezaji mmoja mmoja Azam inawachezaji wakubwa lakini tofauti kidogo itaipa favor Simba.

Msimamo kwenye ligi 

Azam ipo nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 50 baada ya kucheza mechi 24, pointi 11 nyuma ya Yanga (wanaoongoza ligi) na pointi 8 mbele ya Simba ambayo ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 42 baada ya kucheza mechi 17.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here