Home Kitaifa Azam kwa nini mmekubali kuingia huu mtego?

Azam kwa nini mmekubali kuingia huu mtego?

5011
0

Hivi karibuni kumekuwa na taarifa ambazo si rasmi kwamba kuna mambo ya kudhoofishana kimchezo ikiwa ni pamoja na kupuliza dawa kwenye vyumba vya kubadilishia nguo kuelekea katika mchezo husika na uwanja wa taifaumekuwa ukitajwa sana.

Mchezo uliopita wa Simba na Yanga tulishuhudia timu timu zote zikitumia milango ambayo si rasmi kuingia vyumba vya kubadilishia mchezo wa Azam vs Simba pia mambo hayo yamejitokeza.

Mambo haya yanaleta picha na tafsiri mbaya yanapofanyika uwanja wa taifa ambao ndio wenye miundombinu sahihi kwa timu zetu.

Nafikiri hii ni changamoto ambayo wahusika na wadau inabidi waiangalie kwa jicho pana kwa sababu sidhani kama ni jambo jema kuwa linapigiwa kelele kila siku wakati kuna mamlaka husika hazijitokezi kwa ajili ya kulitolea ufafanuzi.

Timu hizi ambazo zinakimbia vyumba vya kubadilishia nguo na kutumia mageti ambayo si rasmi ukiuliza viongozi wanakwambia wanakimbia vyumbani kwa sababu za imani za kishirikina na kukwepa michezo michafu inayofanyika.

Haya mambo sijui yanafanyika muda gani, kwa mfano kupuliza dawa kwenye vyumba vya kubadilishia nguo vitendo hivi vinafanyika muda gani? Nani anaruhusu? Kwa sababu uwanja una uongozi na ulinzi. Ina maana wao ndio wanaruhusu hivi vitu vinafanyika? Kama havipo kwa nini tunakimbilia kwenye imani za kishirikina?

Binafsi sikufurahishwa na kitendo ambacho Azam walikifanya kwa sababu Azam tunaiona kama klabu ya mfano kwa hiyo unapoona klabu aina ya Azam na yenyewe inaingia kwenye huu mtego inabidi uogope.

Azam wakati wanaingia uwanjani kufanya warm-up waliingia kupitia mlango ambao si rasmi wakati wanarudi vyumbani wakapita huko pia. Wakati timu zinaingia uwanjani kwa ajili ya mechi, wachezaji wa akiba na benchi la ufundi wakatokea kwenye mlango ambao si rasmi kwa mara nyingine.

Cha kustaajabisha, wachezaji 11 walioanza kwenye mchezo dhidi ya Simba wakati wa kuingia uwanjani kwa ajili ya mechi wakapita kwenye mlango rasmi. Sasa kama walikuwa wanakwepa uchawi maana yake wachezaji wa akiba ndio wanakwepa uchawi?

Mwisho wa siku Azam ikafa 3-1, sasa cha kujiuliza wamefungwa kwa sababu ya hizo imani za kishirikina au wamefungwa

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here