Home Ligi BUNDESLIGA Ripoti mpya ya Aubameyang na Real Madrid.

Ripoti mpya ya Aubameyang na Real Madrid.

809
0

gazeti2

Moja ya habari ambazo zitatengeneza headline kubwa sana kipindi cha usajili kikifika ni kuhusu tetesi za Aubameyang kuhama Borussia Dortmund.

Story hii imekua ikiandikwa sana na club ambayo inatajwa sana kutaka kumsajili Aubameyang ni Real Madrid. Kama kawaida ya vyombo vya habari vya nchi husika lazima vivutie mchezaji huyu kuhamia kwenye La Liga.

Gazeti la AS la huko Spain lilitoa habari wiki hii kwamba Aubameyang tayari ameshasema Yes kwa Real Madrid kwamba huu ni msimu wa mwisho wa yeye kuwa ndani ya Borussia Dortmund.
Habari hiyo imepingwa vikali na Aubameyang mwenyewe na kusema,“Mimi sasa hivi na focus kwenye msimu huu. Nipo Borussia Dortmund na ndipo ninapofikiria muda wote”.

Kocha wake Thomas Tuchel aliongezea na kusema,“KIla mtu anakubali kwamba Aubameyang ana mkataba wa muda mrefu hapa bila kuwa na uwezekano wa kuhama, Auba ame sign mkataba na anafuraha kuwa hapa. Bado ana amini anaweza kukua binafsi na kama mchezaji”

Kutokana na ukweli huu basi tuendelee ku-enjoy magoli makali ya Aubameyang ndani ya Bundesliga ya Startimes. Weekend hii kocha wao Thomas anarudi kwenye club yake ya zamani kwenye mechi dhidi ya Mainz 05.

gazeti

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here