Home Kimataifa Arsenal yamtengea Perisić mshahara mnono… Maajabu!!

Arsenal yamtengea Perisić mshahara mnono… Maajabu!!

4219
0

Kule London klabu ya Arsenal imahidi kutoa Ofa ya mshahara mnono wa takribani £250,000 kwa wiki, kwa winga wa timu ya taifa ya Croatia na klabu ya Inter Milan Ivan Perisíc endapo atakubali kujiunga na klabu ya Arsenal kwa mkopo.

Washika mitutu hao pia wamemuahidi kama atajiunga nao kwa sasa watampa makataba wa muda mrefu ifikapo mwezi June mwaka huu.

Hata hivyo kuna taarifa zinaeleza kuwa Inter imesema haipo tayari kumwachia Perisic licha ya nyota huyo kuandika barua ya kuomba kuondoka klabuni hapo.

Arsenal ipo kwenye wakati mgumu hasa mara baada ya sakata la Unai na Ozil kushika kasi. Arsenal mpaka sasa tayari Ramsey hayupo kwenye mipango yao hapo msimu ujao.

Ozil yupo matatani na tayari mfumo wa mwalimu haumfai na muda sio mrefu nae atakuwa njia kuondoka Arsenal.

Denis Suarez ambaye alisakwa na Unai kama mrithi wa mikoba ya Ramsey inasemekana anataka kuongeza mkataba mpya mpaka ifikapo 2023.

Je kwanini Arsenal inatoa dau nono kiasi hiki? Shida kubwa ya Arsenal ni mabeki na winga. lakini wapo wapo bize kumfukuzia Perisic kama mbadala wa Ozil. Yawezekana akawa msaada kwa timu kwa sababu hawana winga wa kuaminika mara baada ya Mkhitaryan kushindwa kuonesha makali yake kwa wakati.

Lakini yapo mengi ya kujiuliza sana hapa. Ikumbukwe Perisic hapo awali alisakwa sana na Jose Mourinho lakini klabu ya Man United ilimkataa kwa sababu hakuwa anaendana na sera za usajili za klabu hiyo (Umri-29).

Je Arsenal wao hawalioni hilo? Wachezaji wengi wa Arsenal ukiwaangalia hasa waliokuja hivi karibu wana miaka 30+. Sasa huyu Perisic je? Nina wasiwasi mkubwa na sera za usajili za Arsenal kwa sasa. Yawezekana kuna shida. Kuna taarifa kuwa aliyemwachia Ramsey ni kocha ndiye aliyesema aondoke. Yajayo yanafurahisha.

Nakumbuka niliwahi kuandika hapa kuwa Unai sio kocha wa klabu kubwa. Ni kocha anayewaogopa sana mastaa. Tusubiri tuone lakini ninachokiona hapa mwanamke atakuwa mahari yake

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here