Home Kimataifa Ambundo, Ndayiragije, wapiga bao ligi kuu

Ambundo, Ndayiragije, wapiga bao ligi kuu

3014
0

MSHAMBULIAJI wa timu ya Alliance ya Mwanza, Dickson Ambundo amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Januari wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) msimu wa 2018/2019.

Alliance FC: Aug 2018 >> Oct 2018
🎽Mechi 11:☑️ Ushindi 1, 😊Sare 1, ❌Vipigo 9 (4 mfululizo)
Nafasi 20/19/18

Dec 2018>> Feb 2019
🎽Mechi 9,☑️ Ushindi 5, 😊Sare 4
❌Vipigo 0
Nafasi ya 8

🙌Wow what a Come back


Ambundo ametwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda wenzake wawili, mshambuliaji Ayoub Lyanga wa Coastal Union ya Tanga na kipa Juma Kaseja wa KMC ya Dar es Salaam.

Kamati ya tuzo pia imemchagua kocha wa KMC, Etiene Ndayiragije kuwa kocha bora wa mwezi Januari akiwashinda kocha mkuu wa Alliance, Malale Hamsini na kocha mkuu wa Biashara United, Amri Said alioingia nao fainali.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here