Home Dauda TV Ally Hapi asema Lipuli imefungwa kwa sababu ya hasira, Simba imevunja mwiko

Ally Hapi asema Lipuli imefungwa kwa sababu ya hasira, Simba imevunja mwiko

5792
0

Mkuu wa koa wa Iringa Ally Hapi ni shabiki kindakindaki wa Yanga Chama la Wananchi halafu leo kulikuwa na game Lipuli kutoka mkoa anaoungoza dhidi ya Simba. Nadhani unapata picha namna ambavyo alikuwa anatamani kuona Mnyama anakufa kwenye uwanja wa Samora.

Baada ya Simba kuifunga Lipuli 3-1 Hapi amesema wachezaji wa Lipuli wamefungwa kwa sababu ya hasira zao zilizopelekea kutoka mchezoni lakini pia amesema Simba ilikuwa inapambana kuvunja rekodi ya kutoshinda dhidi ya Lipuli hivi karibuni kwenye uwanja wa Samora.

Sasa kwenye mchezo utakaozikutanisha Lipuli na Yanga mzee baba Ally Hapi atakuwa upande gani? Majibu ameyatoa upitia video hapa chini. Bofya PLAY▶uangalie alivyojibu kuhusu Lipuli vs Yanga.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here