Home DOKUMENTARI Unamshangaa King Kiba? Kuna hawa wengine walioimba na kupiga soka

Unamshangaa King Kiba? Kuna hawa wengine walioimba na kupiga soka

13455
0

Ulimwengu wa soka na mziki nchini Tanzania ulitawaliwa na habari kubwa wiki iliyopita baada ya msanii Ally Saleh Kiba almaarufu kama Ali Kiba kujiunga na timu ya Coastal Union.

Kiba amekuwa akicheza soka la hali ya juu mtaani kwao Kariakoo na katika mechi ya Hisani dhidi ya tema ya Mbwana Samata alionesha uwezo uliomuacha mdomo wazi kila mtu.

Wengi wamekuwa na mtazamo tofauti kuhusu Alikiba lakini Kiba sio mtu wa kwanza kucheza soka pamoja na kuimba muziki, kuba hawa wengine.

Clint Dempsey. Unamkumbuka nyota huyu wa zamani wa Tottenham Hotspur? Sasa huyu Texas anaheshimika kama moja ya marraper wa mji huo na kama unakumbuka mwaka 2006 alichana katika ngoma ya Dont Tread ambayo ilitumiwa na Nike katika kombe la dunia 2006.

Jesse Rodriguez. Nyota wa zamani wa Real Madrid, huyu naye ni rapper mkubwa na wa Latin wanakubali sana nyimbo zake ambapo katika mziki anajiita Jey M, ngima ya Rodriguez iitwayo Lo Sabia ina viwers milion 31 You Tube.

Asamoah Gyan. Kama unakumbuka Gyan alihusishwa na kifo cha rapper wa Marekani Castro, nyota huyu wa Ghana na Castro walikuwa marafiki na wana ngoma yao inaitwa African Girls na Gyan akiwa studio anajiita Baby Jet.

Memphis Depay. Tofauti na wengine, nyota huyu “bishoo” ambaye amewahi kukipiga United yeye ngoma zake ziko studio tu, muda mwingi akiwa likizo anautumia kurap na kama unakumbuka mwaka jana akiachia free style yake ya kwanza na akasema kama sio mpira angekuwa ametoboa katika rap.

John Barnes. Hatukuwepo wakati wa enzi zake lakini Barnes alikuwa nyota wa Liverpool miaka ya 80 na 90, lakini Barnes alikuwa na verse maarufu katika wimbo uitwao World In Motion wa kundi la New Orders nyimbo ambayo ilikuwa maarufu sana miaka ya 90.

Royston Drenthe. Kiungo wa Kiholanzi ambaye wengi tunamkumbuka akiwa Real Madrid na baadaye Everton, nyimbo yake ya Tak Tiki ni marufu Ubolanzi lakini pia ana nyimbo nyingine alimuimbia mwanaye wa kike iitwayo Jemayi Lee.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here