Home Ligi EPL Adui muombee njaa, binadamu sio watu!

Adui muombee njaa, binadamu sio watu!

3561
0

Mashabiki wa Everton FC ya England, wakishangilia moja ya mabao yaliyofungwa na Manchester City dhidi ya timu yao, hapo jana usiku.

Ushindi wa Man City ulimaanisha kwamba mbio za ubingwa zinarudi kuwa ngumu na kuwatia presha zaidi Liverpool ambao ni wapinzani wao wa kitongoji kimoja cha Merseyside jijini Liverpool. Man City walishinda 2-0.

Liverpool ni klabu iliyoanzishwa baada ya mgogoro ulioikumba Everton…kwa hiyo Everton ndiyo mama wa Liverpool FC. Mama akikutakia mabaya, ni laana. Heshimu baba na mama….! IMEWATOKEA KUTOKEA BONGO

Machi 30, 2014, Azam FC na Simba zilikutana kwenye mchezo wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara.

Huu ulikuwa mchezo muhimu kwenye mbio za ubingwa kwani Azam FC waliingia wakiongoza ligi kwa pointi 50, pointi 4 juu ya Yanga iliyokuwa na 46.

Yanga ambao walikuwa na kibarua Mkwakwani Tanga dhidi ya Mgambo (ile mechi ya Mohamed Netto), waliutegemea mchezo huu kuwapunguza kasi Azam FC.
Dakika ya 16, Khamis Mcha Khamis ‘Vialli’ akaifungia Azam FC bao la kuongoza ambapo mashabiki wa Simba waliinuka kushangilia.

Dakika ya 45, Joseph Owino ‘Gera’ akaisawazishia Simba bao. Mashabiki wa Yanga wakainuka kushangilia huku wale wa Simba wakimrushia maneno ya kero mchezaji wao kwa kusawazisha.

Dakika ya 56, John Bocco akaifungia Azam FC bao la pili kwa kichwa cha mkizi akimalizia tiktak ya Kipre Tchetche.

Mashabiki wa Simba wakainuka kwa furaha na kuishangilia Azam FC.

Wakati mambo yakiendelea hivyo, zikaja taarifa kutoka Tanga kwamba Yanga kafungwa 2-1 na Mgambo…mashabiki wa Simba wakaongeza shangwe.

Matokeo hayo yanaifanya Azam itimize pointi 53 baada ya mechi 23, wakati Yanga SC iliyofungwa 2-1 na Mgambo JKT Uwanja wa Mkwakwani, Tanga inabaki na pointi zake 46 baada ya mechi 22.

Mwisho wa msimu, Azam FC wakawa Mabingwa!

© Zaka Zakazi

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here