Home Kimataifa Achana Na Cavs na Warriors, Washington Wizards Dhidi Ya Celtics Ni Vita...

Achana Na Cavs na Warriors, Washington Wizards Dhidi Ya Celtics Ni Vita Muda Wote.

1488
0
WASHINGTON, DC - MAY 04: John Wall #2 of the Washington Wizards celebrates after scoring in the third quarter against the Boston Celtics in Game Three of the Eastern Conference Semifinals at Verizon Center on May 4, 2017 in Washington, DC. Washington won the game 116-89. NOTE TO USER: User expressly acknowledges and agrees that, by downloading and or using this photograph, User is consenting to the terms and conditions of the Getty Images License Agreement. (Photo by Greg Fiume/Getty Images)

Inawezekana ukawa shabiki mkubwa wa Golden State Warriors au Cleveland Cavaliers na ukawa unasubiri mechi yao ya fainali kwa hamu iwapo itatokea. Lakini kamwe usikubali kupitwa na michezo inayoendelea kati ya Houston Rockets vs San Antonio Spurs na Washington Wuzards Vs Boston Celtics.

Mchezo wa Washington Wizards vs Boston Celtics inawezekana ukawa na mvuto zaidi na ushindani mkubwa kutokana na aina ya vikosi vyote viwili huku kwa kiasi kikubwa ikitawaliwa na ubabe na visasi.

Wakiwa nyuma kwa kupoteza michezo 2 mfululizo ambayo walikuwa na uwezo wa kushinda japo mmoja kati yake, Wizards walirejea nyumbani na kushinda mchezo mmoja na kisha alfajiri ya leo wamefanikiwa kushinda  121-102 dhidi ya Boston Celtics na kufanya mchezo huo uwe 2-2. Wakiongozwa na mchezaji anayeonekana kuimarika kila kukicha John Wall, klabu ya Washington Wizards imekuwa ikipata msaada wa Bradley Beal, Markieff Morris na Otto Porter.

“Wizards walinufaika kwa kupata pointi 34 kutokana na Celtics kupoteza mipira kirahisi na Morris, ambaye alikuwa na alama 16 na rebound 10 alisema tunao uwezo wa kufanya yote hawa na kuwafanya wapinzani wafuatane na kasi yetu. Washington walifanikiwa kuipoteza Celtics kwa kufunga mfululizo pointi 26-0 kuelekea katika robo ya 3.

Mchezaji wa Washington, John Wall alikuwa na pointi 27 na pasi na kuwatesa Celtics ambapo katika michezo ya mtoano ameweza kufunga walau pointi 20 na kutoa pasi zaidi ya 7 katika michezo 10 ya mtoano mfululizo, akiwa mchezaji wa kwanza tangu Michael Jordan.

Mchezaji Bradley Beal yeye alifunga alama 29 points.

Isaiah Thomas ambaye alikuwa na pointi 17 katika dakika 15 za mwanzo alikabwa vyema na kumaliza mchezo akiwa na alama 19 tu kwa upande wa Boston Celtics.

HIGHLIGHTS

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here