Home Kitaifa Ndimbo asimukia Ruge na Kibonde walivyomfungulia DUNIA

Ndimbo asimukia Ruge na Kibonde walivyomfungulia DUNIA

2990
0

Clifford Ndimbo ni miongoni mwa watu waliopita na kutangaza kipindi cha michezo ndani ya Clouds FM lakini kwa sasa ni afisa habari wa TFF. Ndimbo amesema Ruge na Kibonde walishiriki katika kumtengeneza hadi kufika alipo sasa.

“Haikuwa wiki rahisi kutokana na kupoteza watu wawili mfululizo ambao hadi hapa nilipofikia wanamchango mkubwa sana kwangu”-Clifford Ndimbo.

“Wakati naingia Clouds FM, Ruge ni moja kati ya watu ambao waliniamini kwa kiasi kikubwa sana na hadi hapa nilipofikia kuna mchango wake mkubwa.”

“Kwa upande wa Ephraim Kibonde, wakati naingia Clouds FM kwenye idara ya habari na michezo yeye ndio alikuwa kiongozi. Mara ya kwanza nasikika hewani kwenye kipindi cha michezo Kibonde ndio alinipa nafasi hiyo.”

“Nakumbuka siku hiyo nilikuwa nimeandaa script kwa ajili ya yeye kwenda hewani kwa sababu nilikuwa miongoni mwa watu tunaoandaa script yeye anakwenda hewani. Siku hiyo wakati namkabidhi script akasema leo unafanya wewe, sikuwa nimewahi kufanya kipindi cha michezo popote ndio kwanza nilikuwa nimetoka chuoni.”

“Baada ya siku ile aliendelea kuniamini na kunipa nafasi. Kwa hiyo ni msiba ambao umenigusa sana kwa sababu hapa nilipofikia mchango wake ni mkubwa sana Ephraim Kibonde lakini pia siwezi kusahu mchango wa Ruge Mutahaba.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here