Home Kitaifa Kauli za watu mbalimbali baada ya kifo cha RUGE

Kauli za watu mbalimbali baada ya kifo cha RUGE

2529
0

“Ruge amekuwa akiishi maisha ya kujitolea yeye ili wanufaike wengi”-Mh. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya nne.

Mchango wake kwangu haupimiki nilipenda maisha yake aliyoishi kuwatia hasira Vijana alikuwa akipenda kusema “Nataka leo niwatie hasira”-Tulia Ackson, Naibu Spika-Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Ruge hakuamini kwamba kuna muda unaoweza kukosa kazi…kila muda ni kazi” anaongea @mwigulunchemba, Mbunge wa Iramba Magharibi.

Licha ya kuwa bado anauguza majeraha aliyoyapata kutokana na ajali ya gari, Mwigulu amefika hapa msibani akichechemea kwa ajili ya kuomboleza kifo cha #RugeMutahaba ambaye alikuwa rafiki yake na mshirika katika kazi mbalimbali.

“Jambo hili ni kubwa kwetu Watanzania, jambo hili ni kubwa kwetu ndani ya Serikali. Hivyo natoa pole kwa Watanzania wote. Nasema hivyo kwa sababu Watanzania wote tunafahamu mchango wake” Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

“Ruge ni mtu ambaye anatamani kuona mabadiliko na anatamani kuona vitu vikiwa kwenye ubora zaidi ya jana” Dkt. Hamisi Kigwangala, Waziri wa Utalii na mali asili nchini Tanzania.

“Ruge alikuwa mtu wa vision na alikuwa anasimamia vision yake, hakuwa mtu wa kuiacha vision yake katikati, ukitoa u-boss Ruge ni rafiki mzuri”-Ajmy Inna, mke wa Mkurugenzi wa Clouds Media Group.

“Kuondoka kwa Ruge ni pigo kubwa sana”-Bi Joyce Mhavile, Mkuugenzi Mtendaji wa ITV na Radio One.

“Ruge amebadilisha maisha ya watu wengisana”-Sebastian Ndege (Jembe ni Jembe).

“Kazi ya Ruge ipo wazi na inaonekana na wengi wameguswa naye”-Zitto Kabwe akiele namna ambavyo ameguswa na msiba huu wa mpendwa wetu Ruge Mutahaba.

“Kifo cha Ruge Mutahaba ni pigo kubwa sana, naamini mambo aliyoyafanya kwa miaka takribani 49 yataendelea kudumu” Tido Mhando.

“Taifa limempoteza mpiganaji maarufu mwenye uwezo mkubwa wa hali ya juu sana…” Mhe. Edward Lowassa ametoa neno baada kuwasili msibani Mikocheni-DSM.

“Ruge ni kiungo mchezeshaji na anamchango mkubwa sana kwenye tasnia yetu” @mrishompoto akieleza namna mchango wa mpendwa wetu Ruge Mutahaba ulivyo kwenye sanaa.

#RugeMutahaba alitoa nafasi kwa viongozi wa #CHADEMA kutumia #CloudsTv kuhamasisha uchangiaji wa michango kwa ajili ya matibabu ya Mbunge #TunduLissu.

Hayo yanaelezwa katika video hii na Mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa akisema hilo ndilo jambo lililomuweka karibu na Ruge.

“Taifa limepoteza mtu mwenye vitu vingi ndani ya nafsi moja” Imani Kajula, Mkurugenzi wa Kampuni ya EAG.

“Ruge kwangu mimi alikuwa mshkaji zaidi, tulikuwa tunazungumza, kubishana, kutofautina na pia tulikuwa tunaweza kukubaliana…” Mhe. Nape Nnauye Mbunge wa Mtama.

“Taifa limepoteza mtu wa muhimu sana” Erick Shigongo Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers.

“Ruge Mutahaba alikuwa mtu wa kusaidia vijana kwa heshima” Julius Mtatiro.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here