Home DOKUMENTARI Huyu ndiye Kocha wa zamani wa Yanga aliye aga dunia

Huyu ndiye Kocha wa zamani wa Yanga aliye aga dunia

7717
0

Mario: nianze na salamu zangu za siku ya kuzaliwa za Jack Chamangwana nimefanya kazi na wachezaji nguli wa soka wengi sana hapa Mobile Motors Limited (kwa sasa Toyota Malawi) na Jack alikuwa mmoja wao. Wengine ni Zorro Msiska, Mustafa Munshi, Robert Kamwendo, Charles Satha, Peter Tsinabuto na Bernard Chirwa. hayo yalkuwa maneno ya Mario.

Chamangwana amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 61. hivi majuzi nahodha huyu wa zamani wa malawi alikimbizwa hospitalini baada ya kukumbwa na shinikizo la damu

Jack amecheza michezo 133 akiwa anashikilia rekodi ya kuwa mchezaji namba mbili aliyecheza michezi mingi. Alianza Mchezo wake wa kwanza ilikuwa mechi ya kirafiki dhidi ya Kenya tarehe 10 July 1975 kule Lilongwe akiwa na miaka 18.

Kikosi cha Kenya

Malawi maarufu kama Flames walishinda kwa mabal 3-1 ikiwa legendi Kinna Phiri alifunfa mabao mawili kabla ya Isaac Muhura kuhitimisha karamu hiyo. Timu ya taifa ya malawi ilikuwa chini ya kocha Mbrazil Bw Moreira, na kikosi chao kilikuwa hivi.

Frank Mlotcha,Steven Phiri, Bosco Munthali, Robert Banda, Jack Chamangwana, Montfort Pemba, Spy Msiska, Kinna Phiri, Yasin Osman, Patrick Chikafa na Isaac Muhura.

Jack alitolewa na kumpisha Elvin Mwafulirwa. Mwaka ule Jack alisafiri na timu yake mpaka nchini Zambia kwenye michuano ya East and Central Africa Senior Challenge Cup (ECASCC). The Flames walifika fainali na kupoteza kwa matutua 2-1 dhidi ya Kenya baada ya sare ya mabao 2-2 wakati wa muda wa nyongeza. Aliccheza michezo saba katika mwaka wake wa kwanza.

Miaka miwili baadae Jack alicheza michezo yote 28 na kufunga bao lake la kwanza kwenye ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Botswana kwenye mchezo wa kirafiki kule Gaborone mwaka 1977. Pia alicheza michezo yote 1980 (13) na 1982 (7). Tarehe 3 Oct 1982, kwenye michuano ya kufuzu ya African Cup of Nations (AFCON) dhidi ya Zimbabwe jijini Harare, Jack alifikisha mchezo wake wa 100 kwenye kikosi cha Malawi ambapo walishinda mabao 2-0.

Miaka miwili baadae katika michuano hiyo ya African Cup of Nations kule Bouake, Ivory Coast mnamo tarehe 08 April 1984, Jack alivunja rekodi ya Kinna Phiri alipofikisha michezo 118 na kuwa mchezaji aliyecheza michezo mingi zaidi. Rekodi yake hiyo ilidumu kwa miaka 7 kabla ya Young Chimodzi kuivunja mwaka 1991.

Jack amefanya kazi chini ya makocha 7 nal ni mbrazili Wander Moreira, Hydri Kondwani, George Curtis, Ted Powell, Alex Masanjala na Henry Moyo kisha kocha wake wa mwisho ni mskochi Danny McLennan.

Jack ni mchezaji wa kwanza kuingia fainali 4 za ECASCC ile ya Lusaka mwaka 1975 Malawi ilipoteza kwa Kenya, nyingine mwaka 1978 Malawi ilipoichabanga Zambia 3-2.

Pia alishiriki katika fainali za mwaka 1979 ilipoifumua Kenya 3-2 magoli ya Bannet Gondwe, Stock Dandize na Collins Thewe.

Mwaka 1984 alishiriki fainali yake ya mwisho ECAS kule jijini Kampala, Uganda, lakini awamu hii Malawi ilipata kipigo cha mbwa mwizi cha mabao 3-0 kutoka kwa Zambia.

Jack alicheza mchezo wake wa mwisho tarehe 16 April 1985 kule Maputo dhidi Mozambique kwenye michuano ya kufuzu African Cup of Nations mechi ya marudiano ambapo Malawi ilipoteza kwa jumla ya mabao 6-5 kwenye mikwaju ya penalti.

Kikosi chao ni

John Dzimbiri, Harry Waya, Ruben Malola, Collins Thewe, Jack Chamangwana, Young Chimodzi, Lawrence Waya, Jonathan Billie, Frank Sinalo, Peterkins Kayira and Clifton Msiya. Dickson Mbetewa na Holman Malunga walitokea benchi Malola na Jack.

Mwaka 1986 Jack aliondoka Afrika Kusini alipoichezea klabu ya Kaizer Chiefs. Alichaguliwa kuwa kocha wa Chiefs mwaka 1988 kabla ya nafasi yake kutwaliwa na Jeff Butler mwaka 1989. Pia aliifundisha Dar Young Africans ya Hapa kwetu Tanzania mwaka 2006.

Jack pia aliwahi kuwa kocha wa malawi 1998 kwa michezo 13 huku akishinda mchezo 1 kudroo 6 na kupoteza 6. Pia alifanya kazi kama Mkurugenzi wa ufundi FAM mwaka 2009 na 2013. Pia mwaka 2010 alikuwa kwenye benchi la ufundi la Malawi katika michuano ya Afcon . Jack yeye na kocha msaidizi Young Chimodzi ndjo wachezaji pekee waliokwenda katika michuano ya Afcon mara mbili kama wachezaji mwaka 1984 na 2010.

Kati ya 2014 2015 alifanya kama kocha msaidizi chini ya kocha mkuu Young Chimodzi timu ya taifa ya Malawi. Amefariki dunia akiwa mkurugenzi wa ufundi wa Befoward Wanderers tokea 2016.

Takwimu zake

Mashindano P W D L F A %

kirafiki 58 32 16 10 106 47 55.2

ECASCC 42 23 9 10 67 42 54.8

ACN QUAL 14 4 5 5 18 16 28.6

WC QUAL 7 2 1 4 6 11 28.6

AAG FINALS 5 0 0 5 4 13 00.0

ACN FINALS 3 0 1 2 2 6 00.0

ZONE VI QUAL 3 2 0 1 7 7 66.7

AAG QUAL 1 1 0 0 2 1 1 00.0

JUMLA 133 64 32 37 212 143 48.1

AAG: MICHEZO YOTE YA AFRIKA

WC: KOMBE LA DUNIA

MWAKA Mechi Goli

1975 7 0

1976 15 0

1977 13 2

1978 19 1

1979 14 1

1980 13 1

1981 15 3

1982 7 0

1983 11 1

1984 14 1

1985 5 0

JUMLA 133 10

Makala hii imeandaliwa na Privaldinho kwenye kitabu cha Mario Antoine kwenye kitabu chake cha Football in Malawi kitakachotolewa mwaka huu mwezi December 2018.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here