Home Kimataifa 5 bora ya comeback zilizowahi kutokea kwenye Champions League.

5 bora ya comeback zilizowahi kutokea kwenye Champions League.

10181
0

Mechi kati ya Barcelona na PSG imeingia kwenye rekodi za Champions League.Barcelona inakuwa timu ya kwanza kufungwa bao 4 kwa 0 katika mchezo wa kwanza lakini baadae kupindua matoke.Ifuatayo ni orodha ya mechi 5 katika Chapions League ambazo timu zilipindua matokeo yasiyotarajiwa.

  1. BARCELONA VS PSG – 2017.

Hii ni mechi ya karibu na ndiyo ambayo kwa sasa kila mtu anaizungumzia.Ni jambo ambalo lilionekana haliwezekani kabisa, katika mchezo wa kwanza pale Ufaransa PSG waliwafunga Barcelona goli 4 kwa sifuri na hii ilionesha wazi mchezo ungeishia hapo.

Tofauti na wengi walivyofikiria, Barcelona waliwasubiri PSG uwanjani kwao huku kocha wao akisema wanaweza kuwafunga 6 Barcelona,wengi waliona Enrique anaota. PSG walifika Nou Camp na matumaini kibao lakini ikawakuta fedheha na maneno ya Enrique yakatimia Barca wanamfunga PSG 6 na kuaonga katika hatua inayofuata ya Champions League.

2. MONACO VS REAL MADRID – 2004 

Wakiwa uwanjani kwao Santiago Bernabeu,Real Madrid waliwapiga Monaco katika mchezo wa kwanza kwa jumla ya magoli 4 kwa 2.

Walipoenda Ufaransa,Raul Gonzalez aliwapatia Madrid goli la ugenini ni ikawa aggeregate ya 5 kwa 2. Dakika 10 baada ya goli la Raul, Monaco walipata goli kabla ya Fernando Morientes aliyekuwa Monaco kufunga lingine na baadae Guilly nae aliwafungia Monaco na hadi mwisho wa mchezo Monaco waliibuka kidedea na ushindi wa magoli 3 kwa 1 na wakafuzu kwa faida ya goli la ugenini.

3. DERPOTIVO VS AC MILLAN – 2004Mch

ezo wa kwanza katika uwanja wa nyumbani wa Ac Millan almanusra itokee kilichomtokea Barcelona lakini Deportivo walipata goli moja na mechi yao ya kwanza kuisha kwa kipigo cha goli 4 kwa 1.

Baadae Ac Millan waliwafuata Deportivo hapo ndipo balaa liliwakuta. Magoli ya Walter Pandiani, Carlos Verlon na Albert Leaque yaliipeleka Deportivo mapumziko wakiongoza goli 3 kwa 0. Kipindi cha pili Gonzalez Fran aliipatia Deportivo goli la 4 na mechi kuisha kwa aggregate ya 5 kwa 4.

4. CHELSEA VS NAPOLI – 2012 

Wakiwa chini ya kocha wao Andre Villas Boas Chelsea walikubali kipigo cha bao 3 kwa 1 kutoka Napoli katika mchezo wa kwanza Italia lakini Chelsea hao hao mechi iliyofuata ya ligi walifungwa na West Bromich ndipo Boas alipotimuliwa na nafasi yake ikichukuliwa na Di Matteo wakati wakiisubiri mechi ya pili na Napoli.

Wakiwa na kocha mpya Di Matteo Chelsea waliikaribisha Napoli Stamford Bridge.

Magoli ya dakika 90 za mwanzo kutoka John Terry,Frank Lampard na Didier Drogba yaliufanya mchezo uende “xtra time”.

Katika dakika hizo za nyongeza Ivanovic alifunga goli dakika ya 104 na mechi na kuifanya Chelsea kufudhu kwa kushinda 4-3.

5. AC MILAN VS LIVERPOOL – 2005 

Hii ni mechi ambayo hakuna shabiki wa Liverpool aneisahau. Lakini tofauti na hizo mechi nyingine hii ilikuwa ni fainali kwa hiyo ilikuwa mechi moja tu. Kipindi cha kwanza kilishuhudia Ac Millan wakiifunga Liverpool magoli matatu na ni wazi wakawa na nafasi kubwa ya kutwaa kombe la UEFA.

Kipindi cha pili magoli ya Xabi Alonso,Vladmir Smicer na kapteni Steven Gerrad yaliifanya iwe 3-3.Baada ya kumalizika kwa sare ilibidi fainali iamuliwe kwa mikwaju ya penati ambapo Liverpool waliibuka kidedea kwa penati 3 kwa 2.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here