Home Uncategorized Kocha mkuu wa Stars atoa ya moyoni kuhusu waliotemwa Stars

Kocha mkuu wa Stars atoa ya moyoni kuhusu waliotemwa Stars

8343
0
SHARE

Siku chache baada ya sintofahamu kuhusu wachezaji waliotemwa katika kikosi cha Taifa Stars, kocha wa timu hiyo Emmanuel Amunike amefunguka kuhusu wachezaji hao.

“Kuna wachezaji waliitwa kujiunga na timu ya taifa lakini kuna maamuzi yalifanyika lakini hiyo haimaanishi wao si sehemu ya timu bado ni sehemu ya timu na wataendelea kuwa sehemu ya Emanuel Amunike, kocha wa timu ya taifa.

“Sote tunafahamu kwenye kila taasisi tunasisitiza nidhamu pamoja na commitment. Jopo la makocha tumeshawaeleza timu ya taifa ni kwa ajili ya kila mtanzania na ni fahari ya watanzania.”

“Wachezaji wa timu ya taifa wanapaswa kuona fahari kwa timu yao na wanapaswa kuja wakiwa wenye matumaini na kujitoa kuona watachangia kitu gani kwenye timu na nina furaha wale ambao tumewaita wako tayari kufanya vizuri siku ya Jumamosi.”

“Kila mchezaji aliyeitwa timu ya taifa ni muhimu na tunaamini ana kitu cha kuchangia kwenye timu kwa hiyo kama kuna mchezaji haumuoni haimaanishi amekataa au hana uwezo.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here