Home Kimataifa Alliance Fc “tutahakikisha hatushuki daraja”

Alliance Fc “tutahakikisha hatushuki daraja”

7181
0
SHARE

Ligi kuu Tanzania bara ni moja ya ligi ngumu hapa afrika Mashariki. Na ni ligi inayofuatiliwa sana.

Baada ya ongezeko la timu 20 kumeonekana wazi kuwa kuna hati hati ya baadhi ya vilabu kuelemewa baada ya matokeo hasi.


Kwa upande wa klabu ya Alliance ya jijini Mwanza wao wanaamini kuwa changamoto ni sehemu tu ya mapito. Bado wana imani na vijana wao.

Kumekuwa na tetesi kuwa vijana wao wachanga wanashindwa kwendana na kasi ya ligi kuu. Msemaji mkuu wa klabu hiyo ametanabaisha mambo kadha wa kadha.

“Ligi daraja la kwanza ni pagumu, na vijana hawa tulipambana nao mpaka kifikia ligi kuu. Nakubali kuwa hiyo ni hoja nzuri lakini ikumbukwe pia wachezaji hawa hawa tumecheza nao madaraja tofauti tofauti na tumefanikiwa. Tunawaamini na kadri muda unavyokwenda watapata uzoefu na jahazi letu litatulia vyema baharini”

“Tutaendekea kupambana na hiki tulicho nacho na hatuwezi kulemaa hata kidogo”


Ni kweli hali ya Alliance sio ya kuridhisha sana hasa baada ya kucheza michezo mitatu na kuambulia alama 1 tu huku ikifunga bao moja pekee na kuruhusu mabao Manne.

01.09. 16:00 Tanzania Prisons Alliance 2 : 0  U  L
27.08. 16:00 Alliance African Lyon 1 : 1  N  D
22.08. 16:00 Alliance Mbao 0 : 1  N  L

“Lengo letu mama ni kuhakikisha hatushuki daraja na nataka kuwaaminisha mashabiki wetu wajue hilo”

“Tunafahamu ligi kuu ni ngumu na tunapambana kadri siki zinavyokwenda, na tunajua tunaweza”


Sakata la ligi kuu kutokuwa na mdhamini pia limechukua sura mpya kwao kwani pia wanaamini hiyo ni moja ya changamoto kubwa kwenye uendeshwaji wa ligi yetu pendwa.

“Ligi kutokuwa na mdhamini ni tatizo, lakini tuna imani watapambana (TFF) kuhakikisha mambo yatakaa sawa. Na tunapongeza jitihada zao katika kuhakikisha mambo yanakaa sawa”

Pia ametoa rai kwa vilabu vingine kitokubweteka na kukomaa kisabuni.

“Sasa ni jukumu la kila klabu kitafuta mdhamini wake na kuongeza mbinu mbadala za mapato kuliko kukaa kimya na kusubiria kuona TFF wanafanya nini maana hiyo kwa ajili ya manufaa yao”


Taarifa na Afisa habari wa Alliance Lucas Mwafulango.


Ratiba ya ligi kuu zifuatazo

Mzunguko wa 4
14.09. 14:00 Mwadui Azam
14.09. 16:00 African Lyon Coastal Union
15.09. 14:00 Lipuli Mtibwa Sugar
15.09. 16:00 Biashara Mara United Kagera Sugar
15.09. 16:00 Kinondoni MC Singida United
15.09. 16:00 Mbao JKT Tanzania
15.09. 16:00 Ndanda Simba
15.09. 16:00 Tanzania Prisons Ruvu Shooting
16.09. 14:00 Mbeya City Alliance
16.09. 16:00 Young Africans Stand U.
Kiporo
25.11. 17:00 Kagera Sugar Young Africans

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here