Home Kimataifa Martial akubali mkataba mpya Old Trafford

Martial akubali mkataba mpya Old Trafford

9090
0
SHARE

Hayawi hayawi sasa mvulana anatarajia kusaini mkataba mpya. Anthony Martial mara kadhaa ameonekana mvulana kwenye mipango ya Jose Mourinho.
Manchester United na Martial wamekubaliana katika mazungumzo ya kuongeza mkataba mpya.

Mfaransa huyu hapo awali aligoma kusaini mkataba mpya baada ya kuonekana kunyimwa nafasi ndani ya kikosi cha Mourinho.

Martial alijiunga na United mwaka 2016 na ameshindwa kuwa na namba ya kudumu Old Trafford tokea Mou ajiunge na klabu hiyo.

Vilabu vya Barcelona, Juventus na Tottenham vilitaka kutumia nafasi ya mgogoro wake na Mou kunasa wino

Mchezaji huyu mwenye miaka 22 anatarajia kusaini mkataba mpya wa miaka mitano kuendelea kuitumikia klabu hiyo.


Kuna taarifa kuwa Mourinho, amepewa mchezo mmoja dhidi ya Burnley katika uga wa Turf Moor kama atapoteza basi atapoteza na kibarua chake.


Mourinho alionesha dhamira ya waziwazi kuwa hamuhitaji Martial lakini bodi ya United ipo tayari kumuongezea Martial mkataba huo mpya.

Taarifa hizi zinazid kuongeza chumvi kwenye taarifa kuwa Mourinho mkurugenzi wa United Ed Woodward, kuwa hawana maelewano mazuri.

Ed Woodward anamhitaji Martial Mourinho hamhitaji Martial. Hii inaonesha mvutano mkubwa sana inadhihirisha kuwa Siku za Mourinho zinahesabika.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here