Home Ligi EPL Tamko la kuhusu uhamisho wa Hazard

Tamko la kuhusu uhamisho wa Hazard

13461
0
SHARE
Dirisha kubwa la usajili nchini Uingereza limeshafungwa tayari. Lilifungwa toka tarehe 9-Agosti lakini klabu zote nchini humo zinaruhusiwa kuuza na sio kusajili. Lakini kwa upande wa nchi nyengine kama Hispania, Ufaransa, Ujerumani na Italia bado hazijafunga dirisha hilo kubwa la usajili. Wao wanafunga tarehe 31-Agosti, hivyo kwa upande wao wanaruhusiwa kusajili kutoka kwenye klabu yoyote haswa kutokea barani Ulaya.
Hiyo inamaanisha bado klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania ina nafasi ya kumsajili nyota wa Chelsea, Eden Hazard.
hazard-chelsea-new-kit
Tayari klabu hiyo imeshafanikiwa kumnasa mlinda mlango kutoka Chelsea, Thibaut Courtois ambaye kwenye mahojiano yake alipotambulishwa na klabu hiyo alisema anaamini ipo siku Hazard ataungana nae klabuni Real Madrid.
Je Hazard ataondoka Chelsea? je kuna nafasi ya kusalia kwa winga huyo? ni baadhi ya maswali ambayo mashabiki wengi wa Chelsea wanajiuliza juu ya hatma ya kumbakiza nyota huyo ambaye amekuwa mchezaji nyota klabuni Chelsea toka aliposajiliwa mwaka 2012 akitokea klabu ya Lille ya nchini Ufaransa
Lakini maswali yote hayo hayaonekani kumuumiza kichwa kocha wa Chelsea, Maurizio Sarri ambapo gazeti moja nchini Uingereza limefichua kwamba kocha huyo hatokuwa tayari kumuuza winga huyo kwasababu kuu moja.
cfcinews-20180818-0001
Inaaminika kwa kocha Sarri amekataa kumuuza Hazard kwa kuwa hana nafasi atakayoweza kuitumia kumsajili mchezaji mwengine atakayeziba pengo la nyota huyo raia wa Ubelgiji.
Gazeti hilo limezidi kueleza kwamba kocha Sarri ameagiza kutopokelewa kwa ofa yoyote ambayo inaletwa klabuni Chelsea akihofia kukosa aina ya mchezaji atakayeziba pengo lake haswa kutokana na dirisha la usajili nchini Uingereza kufungwa.
Kwenye mkutano wa hii leo ambao kocha Sarri amefanya na waandishi wa habari alipoulizwa kuhusu winga huyo mwenye miaka 27, kocha alisema anatazamia nyota huyo ataendelea kubaki Chelsea.
nohazardnoparty-20180824-0001
Kila shabiki wa Chelsea anapiga maombi katika hili swala ili usajili usitokee, kipi kitaendelea? wote tuna subiri…

Taarifa na barnaba wa darajani 1905.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here