Home Kitaifa Dilunga na mikwara kama yote kuelekea mtanange wao vs Prisons hii leo

Dilunga na mikwara kama yote kuelekea mtanange wao vs Prisons hii leo

9009
0
SHARE

Na Tima Sikilo

KIUNGO wa timu ya Simba Hassan Dilunga, ametamba kuendelea kufanya vizuri leo katika mchezo wao wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2018/19 dhidi ya Tanzania Prisons, unayotarajiwa kuchezwa usiku uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Dilunga alisajiliwa na Wekundu wa Msimbazi kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Mtibwa Sugar.

Amesema kikosi chao kipo vizuri na wana uhakika wa kupata ushindi kutokana na maandalizi waliyoyafanya kuelekea katika msimu mpya wa ligi.

Dilunga ameahidi kufanya vizuri katika mchezo huo ili kuendelea kujiwekea uhakika katika kikosi cha kwanza ambacho kinaushindani mkubwa wa namba.

Tumejiandaa vyakutosha na tuna uhakika wa kufanya vizuri, nitahakikisha napambana ili kuendelea kujiwekea uhakika katika kikosi cha kwanza.

Ameongeza kuwa kila nafasi kwake ni ya dhahabu hivyo ataitumia vizuri kuhakikisha anaipatia ushindi timu yake dhidi ya wapinzani wao na michezo yote iliyopo mbele yao.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here