Home Kimataifa Shaffih Dauda kuelekea msimu mpya wa ligi kuu Tanzania

Shaffih Dauda kuelekea msimu mpya wa ligi kuu Tanzania

11693
0
SHARE

Ligi kuu Tanzania bara inataraji kuanza hapo kesho, mambo mengi yametokea hapa katikati lakini kabla filimbi ya kuanza igi yetu kuanza nimeona ni bora niizungumzie.

Nimejaribu kufanya uchunguzi nimeona timu nyingi zina lia ukata, bahati mbaya timu nyingi zinategemea mdhamini mkuu wa ligi kuu na kubweteka zikiamini kwamba atawapatia pesa licha kwamba ilikuwa haitoshelezi lakini walau ilikuwa inawapunguzia mzigo.

Bahati nzuri viongozi wengi wa hivi vilabu ni washkaji zetu tuna mahusiano mazuri, mara kadhaa nimekuwa nikiiwaambia ukweli pamoja na bodi kutopata mdhamini mkuu wa ligi hadi sasa haimaanishi kwamba viongozi wa vilabu wasilaumiwe.

Ni jukumu la viongozi katika level ya vilabu kutafuta partners na wawekezaji, wakati mwingine huu utegemezi unalemaza kwa hiyo baadhi nimewaambia ligi kutokuwa na mdhamini wachukulie kama changamoto kwa sababu wao ndio viongozi na wanajukumu la kuhakikisha hivi vilabu vinaendekea kuwepo.

Ni ngumu kwa mazingira yetu ya kitanzania klabu kufika hatua ya kupata partners wakuweza kusaidia kujiendesha kiuchumi na hili jambo ni pana na linagusa maeneo mengi sana.

Pande zote zinategemeana ndio maana nasema lazima kama wadau tujiweke katika mazingira ya kuangalia kila mdau ana nafasi gani ya kuhakikisha mpira wa nchi hii unasogea na kupiga hatua.

Tumezoea kwamba, shirikisho wao ndio wenye mpira watengeneza sera na kanuni za mashindano, wayekelezaji ni vilabu. Lazima wakae pamoja vilabu na bodi ya ligi na ndio maana kila siku tuna sisitiza ni lazima bodi iwe huru, ijitegemee na iwe na watu wenye uwezo wa kufanya kazi kisiwe chombo cha kinadharia .

Ligi ni jambo kubwa ambalo linatakiwa lijengwe katika misingi ya kuleta imani kwa wawekezaji wanaotakiwa kuja kwa hiyo ukiziangalia hizi timu zote, zipo duni kiuchumi kwa hiyo inaniwia ngumu hata mimi kuwa kwenye nafasi ya kusema timu hizi zipo kwenye nafasi ya kufanya vizuri halafu nyingine hazitafanya vizuri. Ni ngumu, ngumu sana lazima nikiri hilo kwa sababu za kimazingira.

Kwa mfano, hizi timu ambazo zipo kwenye ligi Yanga ni timu kubwa lakini wote ni mashahidi tunaona inavyopambana na ukata, Simba angalau kwa sasa wapo kwenye mood ya kucheza ligi. KMC ni timu ambayo inajiweza kwa maana ya kuwalipa wachezaji, kusafiri kutoka kituo kimoja kwenda kingine na wana uhakika wa kulala na kulipa posho wachezaji.

Timu nyingine ni Azam FC ina uwezo wa kusafirisha wachezaji kuwalipa mishahara na kutimiza mahitaji mengine yote ambayo ni muhimu kwa timu. JKT Tanzania timu ambayo ipo chini ya Jeshi la KujengaTaifa, kusafiri, kulala, kula, kulipa mishahara sio issue.

Mtibwa na Kagera wanapoanza wanakua vizuri sana lakini wanapofika mbele wanapata changamoto za hapa na pale, wana uhakika wa kusafiri lakini uchumi wa wachezaji haujatengemaa. Wanaweza ku-maintain timu icheze lakini sio wachezaji wanufaike kwa kipato na kuwafanya waridhike kucheza mpira wa kiushindani. Tanzania Prisons na Mbeya City pia zipo kwenye kundi hili.

Timu kama Biashara ni ngeni, watu wa Mara wanahamu na ligi lakini watapata changamoto kwa sababu hawana wawekezaji wa kutosha. Itafika wakati watakwama, timu kama Ndanda wote tunajua historia yao.

Mbao licha ya kuwa na udhamini wa GF Trucks & Equipment lakini si mdhamini ambaye anaweza kukidhdi grama zote, Alliance ni timu inayomilikiwa na shule, kusafiri sio issue ni timu ya vijana ambao wamejengwa katika misingi ya kucheza wanaweza kujitahidi wakafanya vizuri.

Kwa mtazamo wangu, vilabu vikubwa vya Simba, Yanga na Azam vitaendelea kushindana juu kupigania ubingwa wa ligi lakini timu kama KMC, JKT Tanzania, Alliance Mtibwa ni timu ambazo zitaleta changamoto.

Timu nyingi ambazo zitaathirika kwa kukosekana kwa mdhamini mkuu, moja kwa moja performance haitakuwa nzuri na zenyewe na viongozi wao wakishindwa kujipanga kutafuta wadhamini zitapata tabu.

Kwa wao kupata wadhamini ni ngumu, ligi inatakiwa iwe imesimama kuanzia organisation, promotion, branding, ili ivutie wawekezaji. Jiulize ligi kubwa inakosa mdhamini mkuu anatoka wapi mtu kwenda kuwekeza kwenye vilabu?

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here