Home Ligi EPL Yaliyojiri EPL, Kane auua mzimu wa August huku kadi ya Vardy kicheko...

Yaliyojiri EPL, Kane auua mzimu wa August huku kadi ya Vardy kicheko kwa Liverpool

11255
0
SHARE

Tottenham 3-Fulham 1. Lucas Moura alitangulia kuifungia Tottenham Hotspur dakika ya 43 na kumfanya kuhusika katika mabao 6(assist 4, magoli 2) tangu ajiunge na Tottenham na pia anakuwa mchezaji wa 46 kutoka Brazil kuwahi kufunga bao EPL.

Aleksandar Mitrovic aliisawazishia Fulham kabla ya Kieran Trippier kuifungia Tot bao la pili kwa mpira wa faulu hili likiwa bao la pili kwake katika EPL tangu Februay 2016.

Harry Kane aliifungia Tottenham bao la 3 na hili linakuwa bao lake la kwanza kuwahi kufunga mwezi wa 8, hii ikiwa ni baada ya mashuti 49 na mechi 15 alizocheza katika mwezi huo.

Everton 2-Southampton 1. Theo Walcot aliifungia Everton goli na kutoa assist ya bao la pili la Richardson na hii ni mara yake ya pili kufunga na kuassist kwenye mechi moja tangu afanye hivyo 2012 akiwa na Arsenal.

Leicester 2-Wolves 0. Jamie Vardy alioneshwa kadi nyekundu na sasa klabu hiyo ndio inaongoza kwa kadi nyekundu Uingereza tangu kocha Claude Puel apewe timu hiyo October mwaka jana(kadi 6).

Kadi ya Vardy ni shangwe kwa mashabiki wa Liverpool kwani atakosa mchezo dhidi ya Liverpool huku nyota huyo akiwa ameifunga Liverpool magoli 7 katika mechi 8 dhidi yao.

Mabao ya Leicester City yalifungwa na James Maddison na lile la kujifunga la Matt Doherty, katika mechi nyingine Newcastle walisuluhu na Cardiff 0-0 huku West Ham wakifungwa na Afc Bournermouth 2-1.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here