Home Kimataifa Hawa Real Madrid msimu hu “Tendrán muchos problemas”

Hawa Real Madrid msimu hu “Tendrán muchos problemas”

8694
0
SHARE

Kama hatujaendelea kichwa cha habari maana yake watapata tabu sana kihispaniola

Baada ya Ramos kufunga lile bao la penati nadhani alihisi amekwisha kumaliza kazi baada ya kuanza kutembea kaama yule mmiliki wa mieleka marekani WWE MacMahon. Staili ile ya kutembea ni maarufu sana ambapo hata Conor Mcgregor aliwahi kuuiga pia.

Diego Costa ameteuliwa kuwa mchezaji bora wa fainali hizi hiki akivunja rekodi ya bao la mapema sekunde ya 46 katika michuano ya UEFArekodi ambayo ilishikiliwa na Paolo Maldini dhidi ya Liverpool mwama 2005.

Madrid ukiwatizama vyema kwa namna wanavyocheza wanacheza kihispanyola sasa tofauti na ule mfumo wa Zidane wa kutafuta matokeo.

Kipindi chote waliochukuwa wanaongoza bado 2 kwa 1 walikuwa wanakaa na mpira zaidi bila kujali kwa zilikuwa zimesalia takribani dakika 20.

Jana Madrid wamepita pasi takriban 837 huku Atletico wakipiga 596. Hii inawerekodi ya pasi nyingi katika kipindi ambavho Zidane alikuwa akiifundisha Real Madrid walipokutana na Atletico. Tukiangali kwa mfano 2016 fainali ya UEFA mchezo ulikwenda takribani dakika 120 lakini Madrid ilizidiwa wingi wa pasi na Atletico kwa kiasi kikubwa tu licha ya wao kubeba ubingwa. Walipga 560 huku Atletico wakipiga pasi 635. Yaan idadi ya pasi za jana ni zaidi 300 zimeongezeka na bado Masrid wamepigwa bao 4 wakati mwaka huu walipokutana na Liverpool fainal ya UEFA walipiga pasi 560 tu na kufanikiwa kufunga mabao 3-1.

Hivyo ni dhahiri aina ya uchezaji ya Zidane sio kukaa na mpira.

Mfumo huu wa pasi unainyima timu nafasi ya kwenda mbele sana na kufanya ushambuliaji kupoa. Mchezo wa mwisho wa Atektico dhidi ya Real, Real walifanikiwa kupiga mashuti 30 na atletico wakipiga mashuti i, jana Madrid wamepiga mashuti 14 tu huku atletico wakipiga 8.

Hawakuamini kama lolote linaweza kutokea. Wameukejeli mfumowa kutafuta mabao na kuuthamini mfumo wa kujizuia kwa kukaa na mpira. Simmeon aligundua Griezmann anatembea kama kiwete. Akagundua kuwa haweza kucheza fujo fujo na Ramos. Akamtoa akamleta Correa ambaye ni mshapu ambaye pia walinzi wa Madrid wasingemhofia na bao la kusazisha limetokana na juhudi zake.

Aliyemuuza Nico Kovacic ajiulize mara mbili kwasababu gani alifanya maamuzi magumu vile. Tumeona jana Casamero alivyoteseka dimba katika kukaba watu wawili ambao wote walikiwa kwenye kiwango bora kabisa (Saul + Lemar)

Bila shida kubwa kubwa ilikuwa hapo pia ndio maana mwisho wa mchezo Casemiro alibeba majukumu makubwa na kuondoka uwanjani akiwa amepiga pasi 41 tu wakati Kroos aliyekuwa huru akipiga pasi 105. Mateso yote alibeba Casemiro maana atletico wao walikuwa wakipata mpira wanalinyookea goli na sio kuuficha mpira.

Saúl Ñíguez’s vs. Real Madrid:

99 amegusa mpira
91% wastani wa pasi
75 pasi
5 alicheza msambamba
4 faulo alizocheza
4 ameondosha hatari
3 ameingilia
1 shuti
1 bao

Sauli alicheza kwa uhuru mkubwa na alikuwa na madhara makubwa katika kila nyanja ya uwanja.

Lemar ameonesha kiwango cha hali ya juu sana. Kwake ujio wa Luke Modric uwanjani bado haukumtisha kabisa. Nadhani ni mmoja kati ua lulu muhimu kwa ATM. Nimesmikia Raisi wao akisema kuwa mwaka huu wana mpango wakufika fainali ya Ucl mwaka huu.

Real Madrid kama wasipofanya usajili msimu watapata tabu sana. Kwa mfumo wao huu mpya wa pasi nyingi wanahitajika kumrudisha James Rodriguez aje abebe dimba lake namba 10 ili Kroos na Casemiro wamalizane na wahuni kama Lemar katikati.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here