Home Kimataifa Moto hauzimi ,”UEFA SUPER CUP” DSTV kesho lakini mimi siwezi kusahau Madrid...

Moto hauzimi ,”UEFA SUPER CUP” DSTV kesho lakini mimi siwezi kusahau Madrid Derby hizi

9341
0
SHARE

Kesho mchezo wa Super Cup ambao ni kama king’ora cha michuano ya UEFA Champions League na Europa unapigwa hapo kesho kwa kuwakutanisha mabingwa wa Champions League Real Madrid vs mabingwa wa Europa Atletico Madrid.

Kuelekea mechi hii itakayopigwa majira ya saa nne usiku pale The Lillekula Stadium Estonia, DSTV wanakuambia moto hauzimi na Super Sports watakuonesha mchezo huu. Kabla ya mechi hii sio vibaya nikakuambia mechi zangu 5 ambazo ziwezi sahau katika Derby hii.

5. Fainali ya Copa Del Rey 2013 Santiago Bernabeu.

Hapa ndio naanza kumjua jua Thibaut Courtois alikuwa kiwango cha juu sana siku hii na huu ukiwa mchezo wa kwanza kwa miamba ya Madrid kukutana katika fainali tangu mwaka 1992, mechi ilikuwa na tensio kubwa sana huku Cr7, Gabi na Mourinho wakila umeme(kadi nyekundu).

Real walikuwa wa moto mno na mara kadhaa lango la Atletico lilikuwa matatizoni huku Benzema na Cr7 wakiongoza mashambulizi lakini uimara wa Courtois aliyekuwa Man Of The Match ukamaliza dakika 90 kwa sare ya 1-1.

Dakika za nyongeza mashabiki wa Madrid hawakuamini macho yao dakika ya 99 pale Miranda alipofunga bao la pili na la ushindi kwa Atletico Madrid na mchezo kuisha kwa matokeo ya 2-1.

2.La Liga 2014 Vicente Calderon.

Wakati hiyo mechi ya kwanza ilikuwa ni Real Madrid walioumia sasa hii ilikuwa zamu ya Atletico Madrid kulia, mechi ilianza kwa Madrid kuwafunga Atletico ndani ya sekunde 180 tu na alikuwa Karim Benzema.

Dakika ya 28 Koke aliisawazishia Atletico na tukaamini half time ni 1-1, aaah wapi dakika ya 45+1 alikuwa Fernandes Arena akafunga la pili kwa Atletico Madrid na mechi ikaenda half time 2-1.

Kipindi cha pili Diego Simeone alijua mashabiki wa Atletico wanajua utamu wa alama 3 kutoka kwa Real Madrid akapaki basi, na hadi dakika ya 80 walifanikiwa kuzuia na kuona wakipata alama 3 lakini dakika ya 82 MRENO Cr7 aliwazima na kuufanya mchezo kuisha 2-2.

3. La Liga 2015.

Aibu kubwa kwa Real Madrid ninayoikumbuka ilikuwa mwaka 2015 pale Vicente Calderon katika mchezo wa La Liga kati ya miamba hii miwili ambapo Real wanakufa bao 4-0.

Dakika 18 tu za mwanzo tayari Cardoso Mendez na Saul walishafunga mabao mawili kabla ya Griezmann na Mandzukic kufunga tena na matokeo kuisha kwa mabao 4 kwa 0 na hii kilikuwa kipigo kikubwa Atletic kuwapa Madrid kwenye La Liga tangu msimu wa 1987/1988.

2. Fainali ya Champions League 2016.

Hii ilikuwa pale San Sirro nchini Italia mwaka 2016 miamba hii miwili ikakutana katika fainali ya Champions League. Walianza Real Madrid kwa goli lililolalamikiwa sana la Sergio Ramos kabla ya Carrasco kuisawazishia Atletico Madrid.

Mpira ulimalizaka kwa suluhu ndipo muamuzi akaamua fainali iamuliwe kwa matuta, tuta la Juanfram liligonga mwamba na kuigharimu Atletico Madrid kabla ya Ronaldo aliyepiga tuta la mwisho kuufanya mchezo kuisha kwa matuta 5-3.

1.Fainali ya Champions League 2014.

Hii ni kati ya mechi ambayo hata unikurupushe saa sita usiku nitaitaha kama mechi mojawapo kali ambayo niliwahi kuiona, Atletico Madrid walikutwa na matokeo yanayouma kuwahi kuyaona.

Godin alifunga dakika ya 36 na goli lilidumu hadi dakika ya 90 na wazi nikaona Atletico ameshamaliza kazi na wanakwenda kubeba Champions League huku Simeone naye akionekana kufurahia matokeo.

Dakika ya 90+3 zikiwa zimebaki sekunde kwa mchezo kuisha Sergio Ramos alivunja mioyo mashabiki wa Atletico kwa kusawazisha, lakini mda wa dakika za nyongeza Atltico hawakuamini kilichowapata.

Gareth Bale dakika ya 110, Marcelo dakika ya 118 na Cristiano Ronaldo dakika ya 120 iliufanya mchezo huu kuisha kwa Real Madrid kuibuka kidedea kwa ushindi wa mabao 4-1.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here