Home UEFA Champions League Wanaowania tuzo za wachezaji bora wa Uefa hawa hapa

Wanaowania tuzo za wachezaji bora wa Uefa hawa hapa

14436
0
SHARE

Wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa kila nafasi uwanjani kwa msimu wa mwaka wa2017/18 wa UEFA Champions League imetolewa.

Real Madrid bado wameendelea kutawala kwenye tuzo za UEFA Champions League

Takwimu kwa namba

Madrid wamepitisha wachezaji 6, ikiwa ni pamoja na  Cristiano Ronaldo aliyekwendaJuventus baada ya kuisaidia Merengues taji la tatu mfululizo la UEFA Champions League kule mjini Kyiv mwezi Mei. Washindi watatajwa kule Monaco mwaka huu 30 August wakati wa upangaji wa makundi ya UEFA.

Washindani 2017/18 wa UEFA Champions League

Makipa: Alisson Becker (Roma, sasa Liverpool), Gianluigi Buffon (Juventus, sasa Paris), Keylor Navas (Real Madrid)

Walinzi: Marcelo (Real Madrid), Sergio Ramos (Real Madrid), Raphaël Varane (Real Madrid)

Viungo: Kevin De Bruyne (Manchester City), Toni Kroos (Real Madrid), Luka Modrić (Real Madrid)

Washambuliaji: Lionel Messi (Barcelona), Cristiano Ronaldo (Real Madrid, sasa Juventus), Mohamed Salah (Liverpool)

Tuzo hizi zilianzishwa makhususi mwaka jana ili kitambua mchezaji bora katika kila nafasi uwanjani kulingana na mafanikio ya klabu yake ndani ya ligi zao. Washindi wa mwaka huu watatajwa sawa na mchezaji bora wa kiume wa  Uefa (UEFA Men’s Player of the Year) na Mchezaji bora wa kike (UEFA Women’s Player of the Year) 

Mgawanyo wa alama kwa kila mchezaji ambao hawajaingia droo ya mwisho

Makipa
4 Marc-André ter Stegen (Barcelona) – 47 alama
5 Thibaut Courtois (Chelsea, now Real Madrid) – 28 alama
6 Ederson (Manchester City) – 26 alama
7 Hugo Lloris (Tottenham) – 18 alama
8 Jan Oblak (Atlético) – 16 alama
9 David de Gea (Manchester United) – 7 alama
10 Sven Ulreich (Bayern) – 5 alama

Walinzi
4 Giorgio Chiellini (Juventus) – 40 alama
5 Dejan Lovren (Liverpool) – 37 alama
6 Virgil van Dijk (Liverpool) – 24 alama
7 Diego Godín (Atlético) – 15 alama
8 Joshua Kimmich (Bayern) – 14 alama
9 Mats Hummels (Bayern) – 13 alama
10 Gerard Piqué (Barcelona) – 10 alama

Viungo
4 Casemiro (Real Madrid) – 40 alama
5 James Milner (Liverpool) – 18 alama
6 Andrés Iniesta (Barcelona, sasa Vissel Kobe) – 16 alama
7 Ivan Rakitić (Barcelona) – 9 alama
8= Isco (Real Madrid), Sadio Mané (Liverpool), Miralem Pjanić (Juventus), James Rodríguez (Bayern) – 6 alama

Washambuliaji
4 Kylian Mbappé (Paris) – 17 alama
5= Edin Džeko (Roma), Harry Kane (Tottenham) – 15 alama
7 Roberto Firmino (Liverpool) – 13 alama
8= Gareth Bale (Real Madrid), Antoine Griezmann (Atlético), Sadio Mané (Liverpool) – 12 alama

Utaratibu ulikuwa vipi?

Walikuwepo makocha 32 wa vilabu vilivyoshiriki 2017/18 UEFA Champions League hatua ya makundi pamoja na waandishi wa habari 55 kutoka nchi za ulaya  (European Sports Media (ESM) group) kutoka kila taifa mmoja mmoja. Makaocha hawakuruhusiwa kupiga kura kwa wachezaji wa timu zao.

Kila kocha alichagua wachezaji wake watatu bora kstika kila nafasi, mchezaji utakayemchagua nafasi ya kwanza atapata alama 5, wa pili 3 na wa tatu anapata alama moja.

Kwa  mfano unaambiwa chagua makipa watatu bora kuanzia wa kwanza mpaka wa tatu

Kwa mfano

1. Aidan alama 5

2. Kick alama 3

3. Dickson Masanja alama 1

Wachezaji watatu wanaopata alama nyingi zaidi huingia kwenye droo ya mwisho

Washindi msimu uliopita

Makipa: Gianluigi Buffon (Juventus)
Mlinzi: Sergio Ramos (Real Madrid)
Viungo: Luka Modrić (Real Madrid)
Mshambuliaji: Cristiano Ronaldo (Real Madrid)

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here