Home Ligi EPL Bakayoko amechana mkeka

Bakayoko amechana mkeka

9341
0
SHARE

Jorginho amejiunga na klabu ya Chelsea. Mashabiki wa Chelsea wameshaanza kumpaka rangi. Wanadai hapotezi pasi hata moja. Sawa sisi yetu macho. Sitaki kusema lolote juu yake nisije nikaonekana mwanga.Lakini nyuma ya daraja inaonekana kuna nguzo imeng’olewa. Inaonekana kuondoka kwa Matic ni sawa na kuondolewa kwa nguzo hiyo. Ingekuwa ni mti tungesema Man United kumchukua Matic waling’oa mti na mizizi yake yote hawajakata shina.Wachezaji wanne wamekwisha nunuliwa ili kuziba shimo aliloacha Matic. Amekuja Rose Barkley, akaja Drinkwater Danny, kabla ya hapo alisajiliwa Tiemoe Bakayoko na hivi sasa Jorginho amejiunga nao. Wote hawa ni kwa lengo ya kutafuta kiungo atakayemsaidia N’golo Kante kwenye dimba la katikati.Bakayoko wakati anatokea Monaco alinunuliwa kwa Euro milion 40. Chelsea walicheza kamari sawa na ile waliocheza Man united kumnasa kinda Anthony Martial kwa dau la Euro 50 lengo ikiwa ni kufanya usajili wa bahati nasibu. Ni bahati nasibu ndio kwa sababu hata kama soko limekua lazima tukubaliane milioni 40 kwa mchezaji ambaye hajacheza mechi 60 ni kurusha jiwe gizani.Kwa united kamari yao tunaweza kusema ilitiki hajachana sana mkeka wao. Inawezekana msimu wa kwanza Martial alirudisha fadhila kwa kufunga mabao 17 na kuwa kinara wa timu. Msimu huu uliopita licha ya kukumbana na matatizo na kocha lakini yeye ndiye mfungaji bora nyuma ya Lukaku kwenye kikosi cha United.Bakayoko amechana mkeka kwa mtazamo wangu mimi. Narudia tena kwa mtazamo wangu mimi. Namuona ameshindwa kuonesha kwamba ufanisi wake ni katika sehemu gan haswa ya uwanja. Antonio Conte amejaribu kulazimisha kumweka Bakayoko kwenye nafasi tofauti tofauti ilimradi tu apate majira ya saa hivi mbovu. Kuna watu wanadai kuwa Bakayoko kuna baadhi ya mechi alicheza vyema. Sawa kubaliana na mimi kuna wakati saa mbovu inakwenda sawa kisha inaoteza tena majira.Lakini Bakayoko amekuja Chelsea kipindi ambacho kwake ni neema. Amecheza takribani mechi 29 akiwa na umri wa miaka 23. Tena kwa kiwango kibovu kile kile. Bila shaka kwake ni neema. Ndio ni neema kwa sababu hajakumbana na ushindani mkubwa.Mwenzie Matic alikuja Chelsea kipindi ambacho hata benchi hakuwa na nafasi. Tena mbaya zaidi alikuja kipindi anatumika kama kiungo mchezeshaji nafasi ambayo Bakayoko anatumika kwa sasa. Miaka ile nafasi hiyo alikuwepo Deco, alikuwepo Yuri, alikuwepo Malouda ambaye ilibidi asukumwe pembeni ilimradi majani yaenee bandani, pia alikuwepo kiungo namba 8 bora kwa wakati wake Frank Lampard achilia mbali akina Kalou. Huyu Matic angecheza wapi? Sasa hivi Bakayoko amekuja kipindi amabcho wapinzani wake ni akina Loftus Cheek huku benchi la Chelsea likiwa na watu kama Kenedy kabla ya kuletwa Drinkwater ambaye nae alifeli.Huyu Bakayoko angekuja kipindi kile hata nafasi ya kiungo mkabaji asingepata hiyo nafasi. Alikuwepo Obi Mikel, alikuwepo Essien na mbaya zaidi alikuwepo kiungo bora wa Ujerumani Michael Ballack. Hata yeye benchi angekaa nani atoke?Bakayoko ametumia mali za marehemu vibaya na mzimu wake utamnyonya damu. Ila kuna wakati nailaumu klabu ya Chelsea kwa kutoa fedha nyingi kwa mchezaji ambaye katika michezo 38 ya Monaco amecheza mechi 20 tu dakika 90 huku akiwa na miaka 21. Binafsi ni kama walibugia pombe za kupewa.Chelsea ya kipindi kile ulikuwa huwezi kupata namba kama huna namba kwenye kikosi cha timu yako ya taifa. Acha Jorginho atuoneshe kama ana hekima ya kuitunza karatasi ya mirathi.Privaldinho (instagram)

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here