Home Uncategorized Nasri sasa kifungoni miezi 18 na sio 6, inaweza kuwa kati ya...

Nasri sasa kifungoni miezi 18 na sio 6, inaweza kuwa kati ya adhabu kubwa katika soka

10882
0
SHARE

Mwanzoni mwa mwaka huu kiungo wa timu ya taifa ya Ufaransa Samir Nasri alikuwa kwenye vichwa vya habari baada ya kukutwa na hatia ya kutumia madawa ya kuchangamsha mwili.

Nasri alifanya tukio hilo akiwa nchini Marekani ambapo baadae alikiri kwamba alifanya tukio hilo kwa bahati mbaya na hakuwa anajua nini kilikuwa kinaendelea kwa wakati huo.

Mwezi February mwaka huu FIFa wakampa adhabu Samir Nasri ya kufungiwa kwa miezi 6 lakini hapo juzi FIFA tena kupitia kitengo chake cha nidhamu wameona adhabu hii haitoshi na wanaiongeza.

Tayari Nasri amekwishaitumikia adhabu yake kwa takribani miezi 6 na sasa itabidi amalizie 12 iliyobaki, hii inaweza kuwa kati ya adhabu kubwa katika soka na kwa haraka haraka tutizame wanasoka wengine ambao wamewahi kukumbana na rungu hili.

Rio Ferdinand. Kocha Alex Ferguson aliingia kwenye mzozo na FA akidai walimuonea Rio Ferdinand kutokana na vipimo vyao, Ferdinand alipewa adhabu ya miezi 8 bila kucheza soka mwaka 2004 na ikamfanya kukosa michuano ya Ulaya.

Sadio Berahino. Huyu ilikuwa juzi juzi tu wakati akienda Stoke kutokea West Brom ambapo vipimo vilionesha amewahi kutumia dawa za kusisimua misuli wakati akikipia West Bromich Albion, akafungiwa kwa wiki 8.

Mamadou Sakho. Hii baadae ilikuja kuleta msuguano mkubwa kati ya UEFA na WADA(World Anti Doping Agency). WADA walipelekea Sakho kufungiwa kwa siku 30 kwa matumizi ya madawa haya lakini baadae UEFA walisema hawajafurahishwa na kitendo cha WADA na hawaamini vipimo vyao.

Jaap Stam. Mchezaji wa zamani wa Manchester United naye mwaka 2001 alikumbwa na gharika hili, inadaiwa Stam alikuwa anatumia dawa hizi akiwa na Lazio na alipokamatwa alifungiwa kwa miezi mitano kucheza soka.

Kolo Toure. Kaka wa Yaya Toure, Kolo alipata adhabu ya miezi 6 wakati akiichezea klabu ya Manchester City mwaka 2011 adhabu ambayo hadi kocha Arsene Wenger alidai kushangazwa nayo kutokana na upole wa Toure.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here