Home Uncategorized Hatimaye Le Bron James atimiza ndoto ya Fid Q

Hatimaye Le Bron James atimiza ndoto ya Fid Q

10874
0
SHARE

Mwanakikapu maarufu duniani kwa sasa Le Bron James ameviteka vichwa vya habari wiki hii baada ya shule yake aliyojenga huku kwao Ohio nchini Marekani kuonekana hadharani.

Kupitia katika foundation yake ya Le Bron James Foundation nyota huyo mpya wa La Lakers ameanza kuchukua wanafunzi 240 katika shule hiyo iitwayo I Promise School.

I Promise School ni shule ambayo wanaosoma hapo wengi ni watoto waishio kwenye mazingira magumu na sii hivyo tu bali atawapa nafasi pia wazazi wao kupata elimu ya juu katika shule hiyo.

Katika shule hiyo wanafunzi watakuwa wakupatiwa uniform za bure, lakini piap masomo ya ziada katika shule hiyo (tution) yatakuwa yanatolewa bure

Si hivyo tu kwani pia Le Bron ana mpango wa kutoa usafiri bure kwa wanafunzi katika shule hiyo huku huduma za chakula nazo(chai, chakula cha mchana na snacks) zitakuwa zinatolewa bila malipo.

Sasa mwanamuziki wa kizazi kipya, legend wa mziki wa Hip Hop Tanzania Fareed Kubanda aka Fid Q amesema kwamba mawazo ya Le Bron James yalikuwa katika kichwa chake.

Kupitia mtandao wake wa Instagram Fid Q aliandika kwamba “Le Bron James amefanya vitu ambavyo mimi nilikuwa ninaviota” akimaanisha aliota kujenga shule kama aliyojenga Le Bron.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here