Home Uncategorized Taarifa za usajili wa Hazard, pamoja na mlinzi anayewindwa na Man United

Taarifa za usajili wa Hazard, pamoja na mlinzi anayewindwa na Man United

9259
0
SHARE

Mambo ni moto huko Camp Nou. Inasemekana viongozi wa Barcelona wamefanya mawasiliano na Eden Hazard na wameshakubaliana kila kitu ni muda wa kujadikiana bei ya mauzo na klabu yake tu. Habati mbaya kwa upande wa Real Madrid.

Klabu ya Everton, inataka kumsajili beki wa Manchester United Marcos Rojo kwa euro milion 30, na Kocha wa Everton Marco Silva anataka kuungana na mchezaji huyo ambaye alimfundisha katika klabu ya Sporting Lisbon

Kocha wa zamani wa walinda lango Kevin Hitchcock ameteuliwa kufanya kazi hiyo hiyo katika timu ya Super Ligi ya India ya Chennaiyin FC -akijiunga na meneja wa zamani wa Aston Villa John Gregory. (Birmingham Mail)

Ngolo kante anatarajia kuongeza mkataba darajani baada ya mabosi wa klabu ya Chelsea kumuahidi ofa kubwa ya mkataba mpya.

Real Madrid haina mpango wa kumsajili mchezaji wa safu ya kati wa Chelsea Willian, mwenye umri wa miaka 29, na wanaemtaka tu ni mlinda lango wa Ubelgiji Thibaut Courtois, mwenye umri wa miaka 26, kutoka the Blues. (marca)

Sakata la Haruna Niyonzima lafika patamu. Baadhi ya wadau wakerwa wadai kuwa tabia yake ya kukosa mazoezini kwa muda ni ya muda mredu tokea kipindi yupo Yanga. Uongozi wamhitaji Niyonzima kufika mbele yao na kueleza tatizo nini.

Meneja wa Leicester Claude Puel amesisitizia tena imani yake kwamba mlinzi wa England Harry Maguire mwenye umri wa miaka 25 – anayechezea Manchester United – atasalia na the Foxes katika msimu mpya. (Sky Sports)

Tarehe kama leo Michael Carrick alitokea Tottenham na kujiunga na Man United

Picha za mchezaji mpya wa Juventus Cristiano Ronaldo alipokutana na wachezaji wenzake.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here