Home Kitaifa Manyika amemtetea Rostand

Manyika amemtetea Rostand

6376
0
SHARE

Baada ya Yanga kupoteza mchezo wao wa marudiano wa kombe la shirikisho Afrika kwa kufungwa 3-2 na Gor Mahia, lawama nyingi zimeelekezwa kwa golikipa Youthe Rostand kwamba ndio alikuwa sababu ya Yanga kupoteza mchezo mechi hiyo uwanja wa Taifa.

Golikipa wa zamani timu hiyo Peter Manyika amemtetea Rostand na kusema golikipa huyo ndiye aliyeibabeba Yanga ilipocheza na Gor Mahia jijini Dar es Salaam.

“Kwa upande wa Yanga kwa sasa golikipa ambaye yupo sawa na anaibeba timu kwa hali iliyonayo bila shaka ni Rostand.”

“Ni kipa mabaye namkubali kwa kila kitu makosa anayofanya na lawama anazopata naona ni za kishabiki. Ukiangalia hata magoli anayofungwa ni wazuiaji ambao wanakuwa wamefanya makosa, anafungwa kwenye nafasi ambazo wafungaji wanakuwa wenyewe.”

“Yeye anajipanga kutokana na nafasi ambayo anatakiwa awepo na anakuwepo kila wakati. Magoli mengi ameokoa na ameiokoa Yanga kwenye magoli ambayo hata angefungwa mimi nisingemlaumu.”

“Kipa ambaye anastahili lawama ni wa Gor Mahia magoli yote mawili yakizembe amesababisha mwenyewe. Magoli ambayo alifungwa Rostand hustahili hata kumlaumu kwa kitaalam.

“Lawama waziangushe kwa timu yao kwa sababu ukiangalia kitaalam walionekana wachezaji wawili tu kati ya wote waliocheza dhidi ya Gor Mahia (Tshishimbi na Rostand) ndio waliweza kuiokoa Yanga wengine wote waliobaki walicheza kawaida.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here