Home Kimataifa Imetajwa sababu Simba kuichagua Uturuki

Imetajwa sababu Simba kuichagua Uturuki

10469
0
SHARE

Rais wa klabu ya Simba Salim Abdallah ‘Try Again’ amesema sababu iliyowafanya kuchagua kuweka kambi Uturuki kwa ajili ya maandalizi ni hali ya hewa ya eneo hilo kurandandana na hali ya hewa ya Dar.

“Uturuki kwa sasa hali ya hewa ipo kama Dar es Salaam, tatizo ni kwamba kunakuwa na mabadiliko ya hali ya hewa. Tupo umbali wa futi 1800 kutoka usawa wa bahari kwenye ile kambi yetu.”

“Hata wanariadha wanapenda kufanya mazoezi kwenye sehemu za miinuko kwa ajili ya kupata pumzi, ukiangalia wanariadha wa Kenya wanafanya mazoezi kwenye milima hata wanariadha wa nyumbani wengi hufanyia mazoezi Arusha kwa hiyo na sisi tumekwenda kwenye muinuko ule kwa ajili ya kupata pumzi.”

“Ni eneo ambalo limetengenezwa maalum kwa ajili ya michezo, mabadiliko ya hali ya hewa mvua kunyesha ni jambo la kawaida lakini hakuna baridi, hali ya hewa ni kama Dar.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here