Home Kimataifa Barack Obama atajwa kwenye kufukuzwa kazi kocha wa Hispania

Barack Obama atajwa kwenye kufukuzwa kazi kocha wa Hispania

9409
0
SHARE

Mwezi uliopita wakati zimebaki siku chache kabla ya kuanza kwa michuano ya kombe la dunia pale Urusi, timu ya taifa ya Hispania ilitawala vyombo vya habari baada ya kumtimua kocha wao.

Julen Lopetegui alifungashiwa virago vyake baada ya kusaini mkataba wa kuifundisha Real Madrid na akatangazwa kuchukua nafasi ya Zinedine Zidane wakati bado anaifundisha Hispania.

Sasa karibia mwezi na zaidi umepita baaada ya tukio hilo na sasa raisi wa chama cha soka Hispania Luis Rubiales ameweka wazi jambo ambalo watu wengi hawakulifahamu wakati wakimfukuza Lopetegui.

Anasema baada ya kumfukuza kocha huyo waliwahi kukutana na raisi aliyepita wa Marekani Barack Obama ambaye kwa maongezi yao anasema Obama anaona alikuwa sahihi kumuondoa Lopetegui wakati ule.

Obama na familia yake walikuwa mjini Madrid wiki chache zilizopita ambako alikutana na waziri mkuu wa Hispania pamoja na raisi huyo wa chama cha soka Hispania na kuzungumza machache ikiwemo syala

Baada ya Lopetegui kutimuliwa, nafasi yake ilichukuliwa na Fernando Hiero lakini Hispania waliishia katika 16 bora, Luis Enrique kwa saaa ndiye kocha mkuu wa timu ya taifa Hispania akichukua mikoba hiyo mapema mwezi huu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here