Home Kitaifa “Yanga haikujiandaa”-Ally Mayay

“Yanga haikujiandaa”-Ally Mayay

7420
0
SHARE

Mchezaji wa zamani wa Yanga na Taifa Stars Ally Mayay amesema klabu hiyo imeshindwa kufanya vizuri kwenye mechi za Caf Confederation Cup kwa sababu haikujiandaa kwa ajili ya mashindano hayo yapili kwa ukubwa katika ngazi ya vilabu Afrika.

“Maandalizi ambayo yalistahili kufanyika kwa ajili ya ukubwa wa mashindano haya hayakufanyika kwa hiyo kwa matokeo ambayo yamepatikana ni kitu ambacho kilikuwa kinatabirika kutokana na namna ambavyo timu ilifanya maandalizi.”

“Si mechi hii ya jana tu, ukiangalia hata maechi ya Nairobi inaonesha tofauti kubwa iliyoonekana kati ya Yanga na Gor Mahia ni maandalizi. Hata fitness level ya wachezaji, uliangalia nafasi ambazo Yanga walikuwa wanapoza au kwenyd eneo la kiungo mtu kama Papy Tshishimbi idadi ya pasi alizokuwa anapoteza ilikuwa ni wastani wa kila pasi mbili pasi moja inapotea.”

“Huo sio wastani mzuri kucheza mpira hususan katika eneo la kiungo, bado utimamu wa mwili wa wachezaji wengi wa Yanga upo chini kwa hiyo ni moja ya viashiria kwamba hawakuwa wamejiandaa.”

“Mechi ya jana wamecheza vizuri hususan kipindi cha pili ukilinganisha na mechi zilizopita. Gr Mahia wameshinda na walistahili kushinda tena kwa magoli mengi. Kama wangekuwa makini na nafasi ambazo walizipoteza wangeweza kufunga hata magoli sita.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here