Home Kimataifa Ni Messi pekee wa kuiokoa Real Madrid katika hili baada ya Ronaldo...

Ni Messi pekee wa kuiokoa Real Madrid katika hili baada ya Ronaldo kuondoka

13870
0
SHARE

Kuondoka kwa Cristiano Ronaldo kutoka Real Madrid kwenda Juventus sio tu kwamba kumeondoa mashabiki wengi wa Madrid ameenda nao Serie A ila kuna jambo jingine kubwa.

Katika wachezaji wa sasa waliobaki mpira ni Ronaldo na Messi ndio ambao wamebeba ballon d’or mara nyingi na bado wana uwezo, lakini Ronaldo ameondoka Real Madrid ila Messi yupo bado Barca.

Sasa sikia hii kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2000(miaka 18) mabingwa mara tatu mfululizo wa Champions League Real Madrid wanaanza msimu mpya wa La Liga bila mchezaji yeyote ambaye amewahi kushinda Ballon d’or.

Kikosi cha sasa cha Real Madrid hakina mchezaji ambaye amewahi kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa dunia na hii mara ya mwisho ilitokea katika kikosi cha Madrid.

Mwaka 1998 Zinedine Zidane alitwaa tuzo ya mchezaji bora wa dunia, na msimu wa mwaka 2000 alikuwepo katika kikosi cha Real Madrid.

Na wakati Zinedine Zidane akiwa Real Madrid ilipofika mwaka 2002 wakati wa dirisha la usajili walimuongeza Ronaldo De Lima ambaye mwaka huo huo mwezi wa 12 akabeba D’or nyingine.

Lakini wakiwa bado hawajatulia, ilipofika mwaka 2004 walimuingeza Michael Owen ambaye naye aliwahi kushinda tuzo hiyo kubwa zaidi barani Ulaya mnamo mwaka 2001 wakati Liverpool ikishinda UEFA.

Wakati Juve wanashushwa daraja mwaka 2006, Madrid walipigia chabo mwanya huo na kuutumia kumuongeza Fabio Cannavaro katika kikosi chao naye akabeba Ballon d’or mwaka huo.

Perez akarudi mwaka 2009 na akaja na mshindo mkuu na safari hii akawaongeza Cristiano Ronaldo na Kaka ambao wote walishawahi kushinda tuzo ya Ballon D’or.

Cristiano Ronaldo alishinda mwaka 2008 huku kaka akishinda mwaka 2007, kwa ujumla hawa ndio nyota ambao wamewahi kushinda Ballon D’or na walikuwepo katika kikosi cha Madrid tangu msimu wa mwaka 2000.

2000/2001 Luis Figo

2001/2002 Zinedine Zidane/Figo

2002/2003 Zinedine Zidane/Figo na Rinaldo De Lima

2003/2004 Zinedine Zidane/Figo na Ronaldo De Lima.

2004/2005 Michael Owen, Zinedine Zidane,Ronaldo De Lima, Luis Figo.

2005/2006 Zinedine Zidane, Ronaldo.

2006/2007 Ronaldo De Lima, Fabio Cannavaro.

2007/2008 Fabio Cannvaro

2008/2009 Fabio Cannavaro

2009/2010 Kaka, Cristiano Ronaldo

2010/2011 Cr7, Kaka

2011/2012 Cr7, Kaka

2012/2013 Cr7, Kaka

2013/2014 Cristiano Ronaldo

2014/2015 Cristiano Ronaldo

2015/2016 Cristiano Ronaldo

2016/2017 Cristiano Ronaldo

2017/2018 Cristiano Ronaldo

2018/2018 ?

Na hii inamaanisha kama Real Madrid wanataka kuuanza msimu ujao wa La Liga na moja ya washindi wa tuzo ya Ballon d’or ni Messi peke yake ndio ana uwezo wa kununuliwa na kwenda kuendeleza rekodi hii.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here