Home Kitaifa MTAZAMO: Shaffih Dauda kuhusu wachezaji wanaogoma kisa mishahara!

MTAZAMO: Shaffih Dauda kuhusu wachezaji wanaogoma kisa mishahara!

8663
0
SHARE

Matokeo ya mechi ya jana Yanga 2-3 Gor Mahia yanautoa Yanga kwenye kombe la shirikisho Afrika (CCC) baada ya sare ya Rayon Sports 1-1 USM Algers katika michezo ya Kundi D.

Gor Mahia wanaongoza kundi wakiwa na pointi 8 sawa na USM Algers lakini Gor ina wastani mzuri wa magoli. Yanga ina pointi moja baada ya kucheza mechi nne, Yanga imebakiza mechi mbili ambazo kama ikishinda zote itafikisha pointi 7 ambazo haziwezi kuisaidia hata kama USM Algers na Gor Mahia zitapoteza mechi zilizobaki.

Ukifuatilia Gor Mahia wana matatizo ya kiuchumi kuliko Yanga. Gor Mahia uchumi wao umetetereka, lakini pamoja na uchumi wao kutetereka wachezaji wanatumia fursa ya mashindano ya Afrika kuonekana kimataifa.

Wachezaji wa Tanzania mara kadhaa mchezaji akiwa hajapata posho, hajalipwa mshahara wake wa mwezi mmoja au miwili ana goma kwenda mazoezini.

Akili yake inavyomtuma, kutokwenda mazoezini anaikomoa timu. Anasahau maisha yake yanategemea kucheza mpira (ndio ajira yake), ili acheze mpira lazima awe fit kwa hiyo anavyogoma kufanya mazoezi anaeathirika ni mchezaji mwenyewe sio timu kwa sababu timu ipo itamtafuta mwingine atakaeweza kuvumilia.

Yanga kushiriki michuano ya kimataifa ilikuwa ni fursa kwa wachezani ambapo walitakiwa kuwa tayari na kujipanga. Matatizo ya viongozi yao waishie kuyaona kwenye vyombo vya habari.

Yanga pamoja na matatizo iliyonayo haishindwi kuiweka timu kambini, kusafirisha timu kwenda kucheza mechi. Wachezaji watakosa huduma za msingi ikiwa ni mishahara na posho ambazo ni hela nyingi lakini vitu vidogovidogo haviwashindi.

Wachezaji wangewekeza nguvu zao kwa kufanya mazoezi timu inapofanya vizuri na wao ndio wanajiuza.

Ngoja nikupe mfano, leo vyombo vya habari vya Tanzania vinamzungumzia Samatta kutakiwa na Levante na Borussia Dortmund. Ukifuatilia story ya Samatta jamaa hajapita kwenye mifumo rasmi ni jitihada zake binafsi.

Kwake fursa ilikuwa ni kucheza na TP Mazembe walipokuja Dar, Samatta alifanya vizuri sana kwenye ile mechi. Mazembe wakavutiwa na uwezo wake wakambeba.

Kama umewahi kufika Lubumbashi utakubaliana na mimi kwamba ni sehemu dauni, huwezi kuifananisha na ilivyo Dar. Kama umezoea kuishi maisha ya kibishoo huwezi kuishi kule.

Huku tunasema viwanja vibovu, ukienda kule Bukavu unakuta mechi za ligi zinapigwa kwenye uwanja una kidongo chekundu lakini Samatta alipita kote huko na kufika alipo sasa hivi. Sasa wachezaji wengi wa kitanzania hawana huo uvumilivu.

Mfano mwingine mzuri, wote tunajua matatizo yaliyomkumba bosi wa TP Mazembe Katumbi kuhusu masuala ya siasa za Congo DR hadi akaamua kukimbia nchi.

Kumbuka yeye ndio boss wa timu, matatizo yaliyompata tungesikia hata timu imeshuka daraja lakini kama timu wanajua Katumbi alikuwepo kwa ajili ya kuwapa kuwatengenezea mazingira ya kufanya vizuri. Performance ya wachezaji uwanjani ndio inaifanya klabu ionekane kwa sababu.

Tangu Katumbi ameondoka Mazembe imeshinda Caf Confederation Cup na kuchukua $1.5m.

Bujeti ya klabu kwa mwaka ni $1m, jumlisha vyanzo vingine timu inaweza kujiendesha. Kama wachezaji wangegoma kwa sababu hawapati tena bonus na posho kama ilivyokuwa mwanzo saizi timu ingekuwa wapi? Pamoja na matatizo wachezaji wa TP Mazembe wakiwa uwanjani huwezi kujua wanachokabiliana nacho nje ya uwanja.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here