Home Kitaifa “Mimi ni kocha wa mpira sio mwalimu wa muziki”-Kocha kuhusu usajili wa...

“Mimi ni kocha wa mpira sio mwalimu wa muziki”-Kocha kuhusu usajili wa Ali Kiba

10417
0
SHARE

Kocha wa Coastal Union Juma Mgunda amesema usajili wa star wa BongoFleva Ali Kiba ni mapendekezo yake kwa sababu anamfahamu na anajua anavuocheza.

Coastal Union imethibisha mumsajili Ali Kiba na tayari yupo kwenye orodha ya safu ya washambuliaji wa timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao wa ligi na mashindano mengine.

“Ali Kiba namfahamu najua anavyocheza, lakini nataka niwaambie watu wa mpira, mimi ni kocha wa mpira sio mwalimu wa muziki, nimemsajili Ali Kiba kutokana na uwezo wake wa kucheza sio kuimba”-Juma Mgunda.

Kiba ameonekana mara kadhaa akicheza mashindano mbalimbali lakini hajawahi kucheza ligi kuu Tanzania bara.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here